https://www.fawaidusalafiya.net
01- Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya tabia za mtoto wa kiislamu
Makala namba 1:
: حُبُّ الْعِلِمُ
Kuipenda elimu (ya kisheria):
: قَالَ رَسُوْلُ اللَّٰهِ صَلَّى اللَّٰه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ-:
{ مَنْ يُرِدِ اللَّٰهُ بِهِ خَيْراً يُفَقِّهْهُ فِي الدِّيْنِ }
Amesema Mtume – swala na salamu za Allah ziwe juu yake: Yule ambaye Allah anamtakia kheri humpa ufahamu katika dini.
رواه البخاري ٧١
[ سلسلة براعم بينونة أخلاق الطفل المسلم – ١ ]
Maelezo:
Mzazi/Mlezi inatakikana amuhimize mwanaye kusoma dini yake, na kumtajia ubora wa hilo na kumtia moyo na hamasa ya kusoma dini yake, kama alivyotuhimiza Mtume – swala na salamu za Allah ziwe juu yake – na maana ya hadithi ni kwamba mtu ambaye Allah anamtakia kheri nyingi basi humpa elimu ya dini na humpa ufahamu wa kuifahamu dini, ufahamu uliosahihi uliojengwa juu ya kutakasa nia kwa ajili ya Allah na matendo mema. Mtume – swala na salamu za Allah ziwe juu yake – humshuhudia yule ambaye amepewa ufahamu katika dini na akaongoka katika uongofu wa Allah, kwamba mtu huyo Allah anamtakia kheri, na anayetakiwa kheri na Allah ameandikiwa wema. Usikose makala namba 2, in Shaa Allah..
Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Imeandaliwa: Tarehe 05/ Jumaadal-ulaa, 1442H ≈ 20/December, 2020M.
Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
JIUNGE NASI TELEGRAM KUPATA FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⤵️ https://t.me/fawaidussalafiyatz •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•