01 – Sharti za tamko: Hakuna muabudiwa anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah

(Sheikh);

Na bila shaka zimejulisha (aya) za kitabu (Qurani) na sunnah hakika (tamko la);

” لَآ إِلَٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ ”

” Hakuna muabudiwa anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah ”

Lina sharti saba, (tamko) hilo halikubaliwi ila kwa (sharti) hizo na hizo (sharti) ni:

1 – Elimu inayopingana na ujinga (kutokujua).

Kiunganishi cha sauti ya Sheikh; https://youtu.be/8uWwPJ1mXf8

Maelezo ya mfasiri:

Anasema Allah – Aliyetukuka-:

{ فَٱعْلَمْ أَنَّهُۥ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ }

{ Basi tambua ya kwamba hapana Muabudiwa anayestahiki kuabudiwa kwa haki ila Allah }.

Katika sharti la kwanza Sheikh anakusudia kuwa na elimu/utambuzi kwamba hakuna yeyote anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah. Na kuwa na elimu ya hilo na kulijua hilo maana yake unakanusha vyote vinavyoabudiwa kinyume na Allah – Aliyetukuka – kama, msalaba, makaburi, mizimu,n.k, na unathibitisha ibada kwa Allah tu.

Kwa hiyo mwenye kulitamka tamko hali ya kuwa hajui maana yake basi halitomnufaisha tamko hilo.

Tutaendelea na Sharti la pili katika makala ijayo In shaa Allah.

Mzungumzaji: Sheikh Abdul-Rrazzaaq Al-badr

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Kiunganishi cha sauti ya Sheikh: https://youtu.be/8gqdDbG087Q

Imeandaliwa: Tarehe 18 – Safar – 1442H ≈ 05 – October – 2020M.

Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kueneza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *