02 – Sharti za tamko: Hakuna muabudiwa anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah

(Sheikh);

Na bila shaka zimejulisha (aya) za kitabu (Qurani) na sunnah hakika (tamko la);

” لَآ إِلَٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ ”

” Hakuna muabudiwa anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah ”

(Sharti la pili);

2 – Na yakini inayopingana na shaka.

Kiunganishi cha sauti ya Sheikh: https://youtu.be/8uWwPJ1mXf8

Maelezo ya mfasiri:

Maana yake hakuna budi kuamini imani ya kukata na uhakika kwa kile kinachojulishwa na tamko hili ambacho ni: ” Hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa ni Allah pekee ” na haitoshi mtu akajua tu bali ni lazima ajue tena elimu ya yakini na kukata na wala asiwe na shaka na kusitasita, kama alivyosema Allah – Aliyetukuka:

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ لَمْ يَرْتَابُوا وَجَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِي سَبِيلِ اللَّهِ ۚ أُولَٰئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ

{ Hakika si vinginevyo waumini ni wale waliomuamini Allah na Mtume wake kisha hawakuwa na shaka (hata kidogo) na wakapigana jihadi katika njia ya Allah kwa mali zao na nafsi zao. Hao ndio wa kweli }

الحجرات (١٥

Ufafanuzi: Katika aya hii Allah ametaja katika sifa za waumini ni kuamini na kutokuwa na shaka yaani kuwa na imani ya kukata moja kwa moja juu ya upweke wa Allah na akataja sifa zao nyingine kisha akasema kuwa hao ndio wa kweli katika imani zao, tena Allah amewaashiria kwa jina la kuashiria watu waliopo mbali ni ishara kuwa watu hawa daraja zao zipo juu na pia maneno haya ameyaleta kwa muundo wa kuyafunga yaani kutokana na daraja walilokuwa nalo kana kwamba hakuna wakweli katika imani zao isipokuwa ni hao. Kwa hiyo yeyote mwenye shaka na kile kinachojulishwa na tamko hili kwa maana hana imani ya kukata, akawa hana uhakika kuwa Allah peke ndiye anayestahiki kuabudiwa kwa haki basi mtu huyo hatonufaika na tamko hili hata akilitamka kwa ulimi wake na pia yule aliyesimama kwa kusema: ” Mimi sisemi kuwa Allah anastahiki kuabudiwa kwa haki, na wala simpingi anayesema ” vile vile huyu si muislamu.

Mzungumzaji: Sheikh Abdul-Rrazzaaq Al-badr Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Imeandaliwa: Tarehe 18 – Safar – 1442H ≈ 05 – October – 2020M.

Kiunganishi: https://t.me/fawaidussalafiyatz

Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz

Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *