صفات الزوج الذي ينبغي أن تختاره المرأة لنفسها.
SIFA ZA MUME AMBAYE ANATAKIWA MWANAMKE AMCHAGUE KWA AJILI YAKE
Makala namba 02:
من هذه الصفات ما يلي:
Miongoni mwa hizi sifa ni (hizi) zifuatazo:
٢ – أن يكون حاملا لقدر من كتاب الله عز وجل على الأقل.
2 – Awe ni mwenye kubeba (kuhifadhi) kiwango (kadhaa) katika kitabu cha Allah – aliyeshinda na kutukuka – kwa uchache zaidi,
فقد زوج النبي – صلى الله عليه وسلم – رجلا من أصحابه بما معه من القرآن كما في “الصحيحين”
Na bila shaka Mtume – swala na salamu ziwe juu yake – alimuozesha mwanaume (mmoja) katika maswahaba wake kwa ile qurani aliyohifadhi kama (ilivyothibiti) katika sahihi mbili.
Maelezo:
Anapokuja yeyote kuchumbia kwenu katika maswali utakayomuuliza ni kuhusu qurani , je amehifadhi chochote katika qurani? akikwambia hajahifadhi chochote katika qurani hata suratul-fatihah! basi tambua huo ni mtihani na hii ni ishara kuwa hata kuswali haswali! Kisa tulichokiashiria hapo juu ni kama kifuatacho: Anasema Sahlu bin Saad Assaaidiy – Allah amridhie: Tulikuwa tumekaa pamoja na Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – basi akamjia mwanamke akimtaka amuoe basi Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – alimwangalia kisha akainamisha kichwa chake, basi pindi aliposimama muda mrefu bila ya Mtume – swala na salamu – kumjibu, akasema mtu (mmoja) katika maswahaba wake: Niozeshe mimi ewe Mjumbe wa Allah, akasema (Mtume): Je unachochote? Akajibu: sina chochote, akamuuliza (tena): wala pete ya chuma. Akajibu: wala pete ya chuma (sina), lakini nitachana shuka yangu hii nitampa nusu na nitachukua nusu. (Mtume) akasema: Hapana, je, unachochote katika qurani? akajibu: Ndio.
(Mtume) akamwambia:
اذْهَبْ فقَدْ زَوَّجْتُكَهَا بما معكَ مِنَ القُرْآنِ.
“ Nenda na nimekuozesha kwa qurani uliyokuwa nayo (uliyoihifadhi) ”
صحيح البخاري ٥١٣٢
itaendelea Allah akitaka, usikose makala ijayo …
Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟ https://www.fawaidusalafiya.net Telegram bonyeza hapa: ☟ https://t.me/fawaidussalafiyatz 🗓️ Imechapishwa: Rajab 14, 1442H ≈ February 26, 2021M,
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾 https://t.me/fawaidussalafiyatz Darsa za ndoa Jiunge hapa: ⤵️ https://t.me/Darasazandoa •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•
السلام عليكم ورحمة الله وبركاته.
Nili kuwa nina suali kuhusu uke wenza. Ikiwa mke ata kuwa na hamu ya mumewe na sio zamu yake, mume ana ruhusika kummtekelezea mke haja yake! Na ikiwa ata tekeleza aki enda kwa mwenye zamu aki shindwa kutekeleza mume ata kuwa hana kosa? Na kama haja tekeleza mke akitoka nje ya ndoa yake kosa ni la nani!!!