03 – Mtiririko/ Mfululizo wa kujifundisha adabu za Mtume wa Allah swala na salamu za Allah ziwe juu yake Makala namba 03:
٣- إطعام الطَّعَام
3 – Kulisha chakula:
عن عبدالله بن عمرو رضي الله عنه، أنَّ رَجُلًا سَأَلَ النبيَّ صَلَّى اللهُ عليه وسلَّمَ: أيُّ الإسْلَامِ خَيْرٌ؟ قالَ: تُطْعِمُ الطَّعَامَ، وتَقْرَأُ السَّلَامَ علَى مَن عَرَفْتَ ومَن لَمْ تَعْرِفْ
Kutoka kwa Abdullah bin Amru – Allah amridhie – kwamba kuna mtu alimuuliza Mtume – swala na salamu za Allah ziwe juu yake – ni tendo gani katika uislamu ni bora zaidi? (Mtume) akasema: Ni kulisha chakula, na kumtolea salamu unayemjua na usiyemjua.
رواه البخاري (١٢)
Maelezo:
Mzazi /Mlezi amfahamishe mwanao kuwa miongoni mwa matendo mema baada ya imani na nguzo za uislamu ni kukithirisha kutoa sadaka ya chakula yaani kulisha chakula masikini, kuwalisha wageni, n.k, kwa sababu chakula ndio kinachotia nguvu katika mwili, na haswa obora huu wa kulisha masikini huwa bora zaidi kipindi cha njaa au bei ya vyakula inapozidi. Na jambo la pili ni kumtolea salamu kila muislamu kwa kutafuta radhi za Allah – aliyetukuka – bila ya kubagua kwa sababu hiyo salamu ni maamkizi ya waislamu wote na ni sababu ya kwanza ya kuungana na ni ufunguo wa kuleta mapenzi, na salamu ni nembo ya dini yetu na katika kutoa salamu ndani yake kuna kudhihirisha unyenyekevu, na kuwaheshimu waislamu, na pia hadithi hii imekusanya wema wa kauli ambao ni kutoa salamu na wema wa vitendo ambao ni kulisha chakula.
Mtiririko huu ni wenye kuendelea Allah akitaka, Usikose namba nne [4].
Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟ https://www.fawaidusalafiya.net Telegram bonyeza hapa: ☟ https://t.me/fawaidussalafiyatz 🗓️ Imechapishwa: Rajab 12, 1442H ≈ February 24, 2021M,
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾 https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/fawaidussalafiyatz •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•
Namshukuru Allah kuifikisha elim Allah akujalien maarifa zaid