03- Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya tabia za mtoto wa kiislamu

03- Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya tabia za mtoto wa kiislamu

Makala namba 3:

الْاجْتِمَاعُ عَلى الطَعَامِ:

Kukusanyika wakati wa kula:

قَالَ رَسُوْلُ اللَّٰهِ صَلَى اللّٰهِ عَلَىيْهِ وسَلّمَ طَعامُ الواحِدِ يَكْفِي الاثْنَيْنِ، وطَعامُ الاثْنَيْنِ يَكْفِي الأرْبَعَةَ

. الراوي: جابر بن عبدالله المحدث: مسلم ( ٢٠٥٩)

Amesema Mtume wa Allah – swala na salamu za Allah ziwe juu yake: Chakula cha (mtu) mmoja kinawatosha wawili na chakula cha (watu) wawili kina watosha (watu) wanne.

Mpokezi ni Jaabir bin Abdullah: Muhaddithi ni Muslim, namba ya hadithi ni (2059)

[ سلسلة براعم بينونة أخلاق الطفل المسلم – ٣ ]

Maelezo:

Mzazi /Mlezi amfundishe mtoto na amuhimize juu ya tabia ya ukarimu na kutoa haswa chakula hata kama ni kidogo ambacho kimeandaliwa kwa ajili ya mmoja basi kitawatosha wawili, na cha wawili kinawatosha wanne na cha wanne kinawatosha wanane, na pia huwenda katika hilo kukapatikana baraka za kwa pamoja. Mzazi /Mlezi amfundishe mtoto tabia ya ukarimu na kutoa mfano unapomnunulia kitu kinacholiwa mwambie mmegee mwenzako au mpe mwenzako kimoja, bila shaka hii itakuwa ni sababu ya kupandikiza ukarimu na tabia ya kutoa katika moyo wake.

Usikose makala namba 4, in Shaa Allah..

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Imeandaliwa: Tarehe 07/ Jumaadal-ulaa, 1442H ≈ 22/December, 2020M.

Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

JIUNGE NASI TELEGRAM KUPATA FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⤵️ https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/Darasazandoa •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *