(Sheikh);
Na bila shaka zimejulisha (aya) za kitabu (Qurani) na sunnah hakika (tamko la);
” لَآ إِلَٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ ”
” Hakuna muabudiwa anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah ”
(Sharti la tatu);
3 – Na ukweli unaopingana na uwongo.
Kiunganishi cha sauti ya Sheikh: https://youtu.be/8uWwPJ1mXf8
Maelezo ya Mfasiri: Maana yake alitamke tamko hili la tauhid kwa ukweli na moyo wake uafikiane na ulimi wake, kwa sababu wanafiki wanalitamka tamko hili lakini nyoyo zao zinapinga na haziamini maana ya tamko hili kama anavyosema Allah – aliyetukuka-:
إِذَا جَاءَكَ الْمُنَافِقُونَ قَالُوا نَشْهَدُ إِنَّكَ لَرَسُولُ اللَّهِ ۗ وَاللَّهُ يَعْلَمُ إِنَّكَ لَرَسُولُهُ وَاللَّهُ يَشْهَدُ إِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَكَاذِبُونَ
{ Pindi wanapokujia wanafiki husema: Tunashudia ya kuwa wewe ni Mjumbe wa Allah. Na Allah anajua kuwa wewe ni Mjumbe wake na Allah anashuhudia ya kuwa hakika wanafiki ni waongo }
سورة المنافقون ١
Ufafanuzi: Wanafiki hawakunufaika na tamko hili la tauhid kwa sababu nyoyo zao zinakadhibisha kile kinachojulishwa na tamko hili na wao hulitamka neno hili kwa uwongo na unafiki. Kwa hiyo mwenye kulitamka neno hili hali ya kuwa anapinga maana na makusudio ya tamko hili basi mtu huyo hatonufaika na kulitamka kwake neno hili kwa sababu ni mnafiki anayedhihirisha uislamu na kuficha ukafiri. Tutaendelea na sharti la nne katika makala ijayo In shaa Allah.
Mzungumzaji: Sheikh Abdul-Rrazzaaq Al-badr
Mfasiri: fawaidusalafiya.net Imeandaliwa: Tarehe 19 – Safar – 1442H ≈ 06 – October – 2020M.
Kiunganishi: https://t.me/fawaidussalafiyatz
Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz
Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•