https://www.fawaidusalafiya.net
(Sheikh);
Na bila shaka zimejulisha (aya) za kitabu (Qurani) na sunnah hakika (tamko la);
” لَآ إِلَٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ ”
” Hakuna muabudiwa anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah ”
(Sharti la nne);
4 – Na mapenzi yanayopingana na kuchukia na kubughudhi.
Kiunganishi cha sauti ya Sheikh: https://youtu.be/8uWwPJ1mXf8
Maelezo ya mfasiri: Ni wajibu kwa muislamu alipende tamko hili na awapende watu wake wanaolifanyia kazi tamko hilo na kulazimiana na sharti zake na ayapende yale yaliyojulishwa na tamko hili na ayachukie yote yanayovunja tamko hili kama ushirikina na ukafiri kwa aina zake mbalimbali, ikiwa ni hivi basi yeyote mwenye kutamka tamko hili kisha akayachukia yale yaliyojulishwa na tamko hili kama vile tauhidi, akawa hapendi kusikia watu wakizungumza tauhidi, hapendi kusikia watu wakikemea ushirikina kama kuabudia makaburi, kuvaa hirizi, kujikinga kwa majini, kwa kifupi mwenye kuichukia tauhidi na akawachukia watu wa tauhidi kwa ajili ya tauhidi waliyoshikamana nayo mtu huyu si muislamu. Kama alivyosema Allah:
وَالَّذِينَ كَفَرُوا فَتَعْسًا لَّهُمْ وَأَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ
{ Na wale ambao waliokanusha upweke wa Allah, basi kuangamia ni kwao na (Allah) atavipoteza vitendo vyao }
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَرِهُوا مَا أَنزَلَ اللَّهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ
{ Hilo ni kwa sababu wao waliyachukia aliyo yateremsha Allah, basi akaviporomosha vitendo vyao }
سورة محمد ٩-١٠
Ufafanuzi:
Allah ameeleza katika aya hizi kuwa wale waliopinga upweke wa Allah yaani waliokufuru hao wameangamia na Allah ameporomosha thawabu za matendo yao ya heri yaani hawalipwi bali yatakuwa ni mavumbi, kwa sababu wao wameichukia qurani ambayo Allah amemteremshia Mtume wake, Allah akaporomosha matendo yao kwa sababu yalifanyika katika misingi ya kishirikina au kikafiri.
Tutaendelea na sharti la tano katika makala ijayo In shaa Allah.
Mzungumzaji: Sheikh Abdul-Rrazzaaq Al-badr Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Imeandaliwa: Tarehe 20 – Safar – 1442H ≈ 07 – October – 2020M. Kiunganishi: https://t.me/fawaidussalafiyatz
Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz
Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•