س: ٥
Swali no. 5:
ماَ هُوَ أَولُ وَاجِبٍ عَلَيْكَ؟
Ni upi wajibu wa mwanzo juu yako?
ج: توحيد الله
Jawabu: Ni kumpwekesha Allah.
سلسلة بطاقات: العقيدة لبراعم الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي
[ Mtiririko wa vikadi: Itikadi kwa chipukizi (vitoto) vya kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy ]
Maelezo ya Mfasiri: Mazazi /Mlezi hapa utamuelezea mtoto maana ya kumpwekesha Allah, maana yake ni kumuabudia Allah peke yake kwa kumpwekesha Allah katika matendo yake na katika ibada zake na katika majina yake na sifa zake;
1 – Kumpwekesha Allah katika matendo yake; hapa utamtolea mifano kama vile kuumba, kutoa riziki, kuendesha ulimwengu n.k,
2 – Kumpwekesha Allah katika ibada zake; hapa utamtolea mifano kama vile kuswali, kuchinja, kujikinga, kuomba dua n.k,
3 – Kumpwekesha Allah katika majina yake kama Arrahmaan, Al-Qudduus, na sifa zake kama kuona, kusikia lakini majina haya na sifa hizi hazifanani na za viumbe bali ni sifa zinazonasibiana na utukufu wake Allah.
Na tauhidi (kumpwekesha Allah) ndio msingi na matendo hayakubaliwi bila ya tauhid ndio maana Allah hakubali matendo ya makafiri na washirikina kwa sababu ya kuuvunja kwao msingi huu.
Usikose makala namba 06 inayofuata in shaa Allah.
Mfasiri: fawaidusalafiya.net Imeandaliwa: Tarehe 30 – Safar – 1442H ≈ 17 – October – 2020M. Tembelea website yetu: ⇩⇩ https://www.fawaidusalafiya.net
Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz
Kupata darasa za ndoa jiunge nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/Darasazandoa
Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•