https://www.fawaidusalafiya.net
(Sheikh);
Na bila shaka zimejulisha (aya) za kitabu (Qurani) na sunnah hakika (tamko la);
” لَآ إِلَٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ ”
” Hakuna muabudiwa anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah “
(Sharti la tano);
5 – Kunyenyekea (kujisalimisha) kunakopingana na kuacha /kupuuza.
Kiunganishi cha sauti ya Sheikh: https://youtu.be/8uWwPJ1mXf8
Maelezo ya Mfasiri:
Maana yake ni ukiwa umekiri na kushuhudia kuwa: ” hakuna muabudiwa anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah “, basi unatakiwa ujisalimishe kwa kumpwekesha Allah na kumuabudia yeye peke yake na ufuate hukumu za uislamu na sheria zake, viungo vyako vitekeleze ibada, kama alivyosema Allah – aliyetukuka:
وَمَن يُسْلِمْ وَجْهَهُ إِلَى اللَّهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ
{ Na mwenye kuulekeza uso (muelekeo) wake kwa Allah na hali ya kuwa ni mwema (mwenye kufuata sheria), basi bila shaka amekamata fundo lililo madhubuti (uislamu) }.
لقمان ٢٢
Ufafanuzi:
Katika aya hii Allah – aliyetukuka – amesema: Mwenye kuelekeza uso wake maana yake mwenye kunyenyekea na kujisalimisha kwa kumtegemea Allah, kwa kumkusudia Allah na kwa kumuomba Allah na kwa yote yawe kwa Allah, na hali ya kuwa ni mtu mwenye kufuata sheria yaani mwenye kumpwekesha Allah na kumuabudia Allah pekee na mwenye kufuata mwenendo wa Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie -, atakuwa amekamata fundo madhubuti yaani amekamata uislamu, kwa maana amekamata tauhidi sawa sawa. Kwa hiyo tunajifunza kuwa yeyote mwenye kutamka tamko hili na akajua maana yake lakini akawa hataki kunyenyekea na kujisalimisha kwa kutekeleza haki za tamko hili na yale yanayomlazimu kama vile kumuabudia Allah na kuzifanyia kazi sheria za kiislamu, akawa yeye anafanya yale yanayoamrishwa na matamanio yake au akafanya yale ambayo yanampatia starehe za dunia pamoja na kuwa hayaendani na uislamu, mtu huyu hatonufaika na chochote na tamko hili.
Tutaendelea na sharti la sita katika makala ijayo In shaa Allah.
Mzungumzaji: Sheikh Abdul-Rrazzaaq Al-badr
Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Imeandaliwa: Tarehe 21 – Safar – 1442H ≈ 08 – October – 2020M.
Kiunganishi: https://t.me/fawaidussalafiyatz Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz
Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•