https://www.fawaidusalafiya.net
(Sheikh);
Na bila shaka zimejulisha (aya) za kitabu (Qurani) na sunnah hakika (tamko la);
” لَآ إِلَٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ ”
” Hakuna muabudiwa anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah ”
(Sharti la sita);
6 – Kukubali kunakopingana na kukataa.
Kiunganishi cha sauti ya Sheikh: https://youtu.be/8uWwPJ1mXf8
Maelezo: Anatakiwa ayakubali yote yaliyojulishwa na tamko hili kwa ulimi wake na moyo wake na aamini kuwa yote ni haki na uadilifu, kwa maana asikikatae chochote kilichojulishwa na tamko hili. Kwa hiyo yeyote mwenye kulitamka tamko hili na akawa hajayakubali baadhi ya yale yaliyojulishwa na tamko hili ima kwa kiburi au husuda au kujiona basi ajue kuwa tamko hili halitomsaidia chochote. Anasema Allah – aliyetukuka:
إِنَّهُمْ كَانُوا إِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا إِلَٰهَ إِلَّا اللَّهُ يَسْتَكْبِرُونَ (٣٥)
{ Bila shaka hao walikuwa wanapoambiwa (dunia): hapana muabudiwa anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, (walikuwa) wakijivuna }
وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُو آلِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍ (٣٦)
Na wakisema: Hivi sisi tuiache miungu yetu kwa ajili ya huyu mshairi mwendawazimu?
سورة الصافات
Ufafanuzi: Hivi ndivyo walivyokuwa washirikina na makafiri na mpaka leo hii wakiambiwa waachane na ushirikina wao na ukafiri wao hujivuna na kuleta kiburi kwa kukataa kukubali upweke wa Allah na vile vile huwafanyia kiburi wale wanao waambia, na husema tena kwa msisitizo kuwa wao hawatoacha ushirikina na ukafiri wao kwa ajili ya mshairi na mwendawazimu yaani wanamkusudia Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – kutokana na ukafiri wao wakampachika sifa hizi ili wasiifuate haki na kuwazuia wengine, na pia huwapachika sifa mbaya kila mwenye kulingania upweke wa Allah. Kutokana na haya ifahamike kuwa: Yeyote ambaye hakubali kuwa Allah pekee ndiye anayestahiki kuabudiwa na katika kukataa hilo ni mtu kukataa kuhukumiwa na sheria ya Allah kwa kiburi na anaingia yule ambaye hakubali upotevu wa dini za kishirikina kama vile waabudia masanamu au makaburi au Mayahudi au Manaswara au dini nyinginezo akawa anasema kuwa: Dini zao ni sahihi au tumetofautiana njia lakini wote tunamuabudia Mola mmoja, yaani kwa kifupi yule ambaye hakukubali yale mafundisho yanayopatikana katika tamko hili ya kuitakidi kuwa dini zote ni za upotevu, dini zote za kishirikina na kikafiri ni za upotevu, dini ya haki ni uislamu tu. Asiye amini haya huyo si muislamu. Tutaendelea na sharti la saba katika makala ijayo In shaa Allah.
Mzungumzaji: Sheikh Abdul-Rrazzaaq Al-badr
Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Imeandaliwa: Tarehe 22 – Safar – 1442H ≈ 09 – October – 2020M.
Kiunganishi: https://t.me/fawaidussalafiyatz Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz
Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•