07- Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya tabia za mtoto wa kiislamu

Makala namba 7:

العَفْوُ والصَّفْحُ:

Kusamehe na kutopatiliza:

قَالَ رَسُوْلُ اللَّٰهِ صَلَى اللّٰهِ عَلَىيْهِ وسَلّمَ

Amesema Mtume wa Allah – swala na salamu za Allah ziwe juu yake:

(لَيْسَ الشَّدِيدُ بِالصُّرْعَةِ، إِنَّمَا الشَّدِيدُ الَّذِي يَمْلِكُ نَفْسَهُ عِنْدَ الْغَضَبِ)

البخاري:( ٦١١٤)

“Hakuwa mwenye nguvu ni yule mwenye kuwapiga watu mieleka, hakika si vinginevyo mwenye nguvu ni yule ambaye anaimiliki (anaizuia) nafsi yake wakati anapokasirika”

Bukhari hadithi namba (6114).

[ سلسلة براعم بينونة أخلاق الطفل المسلم – ٦ ]

Maelezo:

Mzazi /Mlezi muelezee mwanao: kuwa na nguvu si kuwa na mwili mkubwa misuli minene na kuwa na uwezo wa kuwaangusha watu kwa kuwapiga mieleka kwa sababu sifa hii hata baadhi ya wanyama wanayo, bali mwenye nguvu iliyokamilika, mwenye nguvu haswa ni yule ambaye ana uwezo wa kuizuia nafsi yake pindi anapokasirika na akajizuia kutukana, kupiga, kusonya kama waswahili wasemavyo: Hasira ni hasara, kwa hiyo mtu shupavu ni mwenye kuizuia nafsi yake kutokana na kulifanya jambo baya na kama kakasirishwa na mtu basi akaizuia nafsi yake na akamsamehe aliyemkosea.

Usikose makala namba 8, in Shaa Allah..

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Imeandaliwa: Tarehe 13/ Jumaadal-ulaa, 1442H ≈ 28/December, 2020M. Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

JIUNGE NASI TELEGRAM KUPATA FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⤵️ https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/Darasazandoa •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *