https://www.fawaidusalafiya.net
(Sheikh);
Na bila shaka zimejulisha (aya) za kitabu (Qurani) na sunnah hakika (tamko la);
” لَآ إِلَٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ ”
” Hakuna muabudiwa anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah “
(Sharti la saba);
7 – Ikhlaswi /Kutakasa matendo kunakopingana na ushirikina.
Kiunganishi cha sauti ya Sheikh: https://youtu.be/8uWwPJ1mXf8
Maelezo ya Mfasiri:
Kinyume na kutakasa ibada zote kwa ajili ya Allah ni kumshirikisha Allah, kwa hivyo mwenye kulitamka tamko hili na hali ya kuwa hajaachana na ushirikina basi tamko hili halitomnufaisha kwa sababu katika sharti za tamko hili ni kuachana na ushirikina, akiwa anamshirikisha Allah ushirikina mkubwa kama vile kuabudia Makaburi, majini, n.k mtu huyu atakuwa si muislamu. Na vile vile ni wajibu kuzisafisha ibada zote kutokana na taka taka na uchafu wa ushirikina wa aina zote, kama alivyosema Allah:
{ فَاعْبُدِ اللَّهَ مُخْلِصًا لَّهُ الدِّينَ }
{ Basi muabudie Allah hali ya kumtakasia ibada }
الزمر: ٢
Ufafanuzi:
Yeyote mwenye kumshirikisha Allah tamko hili halitomnufaisha ila akitubu na kurudi kwa Allah na kuachana na ushirikina.
Sharti hili la saba ndio la mwisho na sharti hili katika sauti ya Sheikh amepitiwa hajalitaja. Itaendelea in shaa Allah.
Mzungumzaji: Sheikh Abdul-Rrazzaaq Al-badr Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Imeandaliwa: Tarehe 23 – Safar – 1442H ≈ 10 – October – 2020M.
Kiunganishi: https://t.me/fawaidussalafiyatz Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz
Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•