https://www.fawaidusalafiya.net
(Sheikh);
Na bila shaka zimejulisha (aya) za kitabu (Qurani) na sunnah hakika (tamko la);
” لَآ إِلَٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ ”
” Hakuna muabudiwa anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah ”
Hizi sharti za ” Hapana muabudiwa anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah ” amezikusanya mmoja wa wanachuoni katika baadhi ya beti akasema:
Na kwa sharti saba limefungwa (tamko hilo)…
Na katika maneno ya wahy yamekuja kwa haki.
Hakika hali ilivyo hatonufaika msemaji wake … kwa kulitamka isipokuwa pale atakapokamilisha ..
Elimu na yakini na kukubali…
Na kunyenyekea, basi tambua ninayoyasema.
Na ukweli na kutakasa matendo na mapenzi …
Akuwafikishe Allah kwa yale anayoyapenda..
Kiunganishi cha sauti ya Sheikh: https://youtu.be/8uWwPJ1mXf8
Maelezo ya Mfasiri:
Hizi ni beti ambazo zimekusanya sharti saba za tamko hili la: ” Hakuna muabudiwa anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah” Na aliyezitaja beti hizi ni Sheikh Haafidh Al-hakamiy – Allah amrahamu – katika ” Sullam l-wusuul ”
Kuna baadhi ya wanachuoni wameongeza sharti ya nane ambayo ni kukanusha vyote vinavyo abudiwa kinyume na Allah na kujitenga navyo kwa maana hauwi muislamu mpaka ujitenge mbali na ushirikina na washirikina na ukafiri na makafiri na uitakidi upotevu wa dini zao na uuchukie ushirikina na watu wake na uitakidi kuwa wao ni washirikina au makafiri na kupambana nao kama sharti za jihadi zitatimia. Lakini baadhi ya wanachuoni wanaona kuwa sharti ya ikhlaswi inakusanya sharti hii ya nane kwa maana kuitaja sharti ya nane ni katika ukamilifu zaidi.
Huu ndio mwisho wa mfululizo wa makala hizi za sharti za tamko hili.
Mzungumzaji: Sheikh Abdul-Rrazzaaq Al-badr Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Imeandaliwa: Tarehe 24 – Safar – 1442H ≈ 11 – October – 2020M.
Kiunganishi: https://t.me/fawaidussalafiyatz Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz
Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•