10- Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya tabia za mtoto wa kiislamu

10- Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya tabia za mtoto wa kiislamu

Makala namba 10:

الأَمَانَةُ:

Uaminifu:

قَالَ رَسُوْلُ اللَّٰهِ صَلَى اللّٰهِ عَلَىيْهِ وَسَلّمَ

Amesema Mtume swala na salamu za Allah ziwe juu yake

أَدِّ الْأَمَانَةَ إلَى مَنِ اىْٔتَمَنَكَ،وَلَا تَخُنْ مَنْ خَانَكَ

Tekeleza amana kwa yule aliye kuamini wala usimfanyie khiyana yule aliyekufanyia khiyana.

رواه أبو داود ( ٣٥٢٥)

[ سلسلة براعم بينونة أخلاق الطفل المسلم – ١٠ ]

Maelezo:

Mzazi /Mlezi inatakikana umfahamishe mwanao kuwa uaminifu ni tabia njema katika tabia ambazo uislamu imezihimiza na umemsifu yule mwenye kupambika nayo, na maana ya hadithi hii ni kuwa mwenye kuweka amana kwako unatakiwa umpe pindi atakapoihitaji na wala usimfanyie khiyana kwa kulipiza khiyana aliyokufanyia wewe bali umsamehe na umfanyie muamala mzuri. Na amana si mali tu pekee bali hata katika maneno na mazungumzo ikiwa mtu atakusimulia maneno na ukajua kuwa ni siri baina yenu sawa sawa akikwambia hilo au ukajua kwa ishara basi unatakiwa maneno hayo usimwambie mtu.

Usikose makala namba 11, in Shaa Allah..

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Imeandaliwa: Tarehe 22/ Jumaadal-ulaa, 1442H ≈ 06/ Jan, 2021M. Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

JIUNGE NASI TELEGRAM KUPATA FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⤵️ https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/Darasazandoa •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *