س: ١١
Swali no. 11
مَا هِيَ مَخْلُوْقَاتُ اللّٰهِ؟
Ni vipi hivyo viumbe vya Allah?
ج: مِنْهَا: الشَّمْسُ والقَمَرُ والأرْضُ والسَّمَاءُ
Jawabu: Miongoni mwa hivyo (viumbe) ni: Jua na Mwezi na Ardhi na Mbingu.
سلسلة بطاقات: العقيدة لبراعم الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي
[ Mtiririko wa vikadi: Itikadi kwa chipukizi (vitoto) vya kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy ]
Maelezo ya Mfasiri:
Hapa mzazi /Mlezi utamuelezea mtoto katika viumbe vikubwa ambavyo Allah ameviumba na vina maslahi makubwa katika ulimwengu ni Jua na Mwezi na lau Jua likijificha likawa halijachomoza basi bila shaka ulimwengu utapata madhara na maisha ya watu yataharibika. Jua ndiyo sababu ya baadhi ya mimea kujitengenezea chakula, umeme wa jua na manufaa mengine mengi ambayo mengi yao wanayafahamu watu wa elimu ya anga (astronomy), na mwezi unafaida nyingi kama vile kujua nyakati za ibada, funga na haji na nyingine mbalimbali, na pia katika viumbe vikubwa ni mbingu na ardhi na vile vilivyomo humo katika ardhi kuna wanadamu, milima ,wanyama, bahari n.k, na pia huko juu kuna sayari mbalimbali na kuna nyota mbalimbali kama Jua, Mwezi n.k .
Usikose makala namba 12 inayofuata in shaa Allah.
Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Imeandaliwa: Tarehe 16 – Rabi’u-Awwal – 1442H ≈ 02 – November – 2020M.
Tembelea website yetu: ⇩⇩ https://www.fawaidusalafiya.net
Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz
Kupata darasa za ndoa jiunge nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/Darasazandoa
Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•