س :١٣
Swali no: 13
مَا هُوَ الشِّرْكُ؟
Ushirikina ni nini?
ج
Jawabu:
هُوَ عِبَادَةُ غَيْرِ اللّٰهِ
Shirki ni kumuabudu asiyekua Allah.
سلسلة بطاقات: العقيدة لبراعم الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي
[ Mtiririko wa vikadi: Itikadi kwa chipukizi (vitoto) vya kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy ]
Maelezo ya Mfasiri:
Mzazi /Mlezi hapa utamuelezea mtoto maana ya ushirikina Ushirikina: Ni kujaalia kitu katika haki ya Allah ukampa mwingine. Mfano: Ibada zote ni haki ya Allah – aliyetukuka, Mfano dua ni ibada na ibada ni haki ya Allah yeyote atakayeipeleka haki hii kwa kiumbe atakuwa amemshirikisha Allah, kama vile yule mwenye kumuomba maiti au kaburi, kuchinjia majini na mashetani kwa kujikurubisha kwao au kuweka mazindiko katika majumba na mahali pa biashara, kujikinga kwa asiyekuwa Allah, kumtegemea asiyekuwa Allah n.k, na dhambi hii ya ushirikina na ukafiri ni dhambi pekee ambayo mtu akifa nayo hatosamehewa. Usikose makala namba 14 inayofuata in shaa Allah.
Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Imeandaliwa: Tarehe 18 – Rabi’u-Awwal – 1442H ≈ 04 – November – 2020M.
Tembelea website yetu: ⇩⇩ https://www.fawaidusalafiya.net
Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz
Kupata darasa za ndoa jiunge nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/Darasazandoa
Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•