14- Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya tabia za mtoto wa kiislamu

14- Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya tabia za mtoto wa kiislamu

Makala namba 14:

صَّلَاةُ الْجَمَاعَةِ:

Swala ya jamaa:

قَالَ رَسُوْلُ اللَّٰهِ صَلَّى اللّٰهُ عَلَىيْهِ وَسَلّمَ:

Amesema Mtume wa Allah – swala na salamu za Allah ziwe juu yake:

” صَلَاةُ الْجَمَاعَةِ أفْضَلُ مِنْ صَلَاةِ الْفَذِّ بِسَبْعٍ وَعِشْرِيْنَ دَرَجَةً ”

Swala ya jamaa ni bora zaidi ya swala ya mtu pekee kwa daraja ishirini na saba.

رواه مسلم (٦٥٠)

[ سلسلة براعم بينونة أخلاق الطفل المسلم – ١٤ ]

Maelezo:

Mzazi /Mlezi mfahamishe mwanao wa kiume ubora wa swala ya jamaa pindi atakapofikia umri wa kupambanua na utakapoanza kumuamrisha swala na ongoza naye pindi unapoenda msikitini na mfahamishe ubora wa swala hii ya jamaa juu ya swala ya aliyeswali peke yake katika malipo, anayeswali jamaa humzidi yule anayeswali peke yake kwa daraja 27 na pia katika riwaya nyingine humzidi kwa daraja 25, na hii tofauti ya daraja hutokana na ubora wa kuitekeleza hiyo swala kama vile unyenyekevu katika hiyo swala, wingi wa jamaa, utukufu wa mahali anaposwali, kwa ajili hii wengine hupata daraja 27 na wengine 25.

Usikose makala namba 15, in Shaa Allah.. Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Imeandaliwa: Tarehe 02/ Jumaadal-aakhir 1442H ≈ 15/ Jan, 2021M.

Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

JIUNGE NASI TELEGRAM KUPATA FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⤵️ https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/Darasazandoa •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *