س: ١٦
Swali no. 16:
مَنْ هُمْ الْمَلَاءِكَةُ؟
Ni nani hao Malaika?
ج:
Jawabu:
هُمْ خَلْقٌ خَلَقَهُمُ اللََّٰهُ مِنْ نُوْرٍ.
Hao (Malaika) ni viumbe (ambavyo) ameviumba Allah kutokana na nuru.
سلسلة بطاقات: العقيدة لبراعم الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي.
[ Mtiririko wa vikadi: Itikadi kwa chipukizi (vitoto) vya kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy ]
Maelezo ya Mfasiri:
Hapa Mzazi /Mlezi atamueleza mtoto kwamba Malaika ni viumbe wa Allah na wameumbwa kutokana na nuru na hawamuasi Allah, siku zote na muda wote wapo katika ibada na Malaika ni wengi kuliko wanadamu.
Imani ya kuamini Malaika kwa ujumla inakusanya kuamini mambo manne (4);
1 – Kuamini Majina yao kwa wale tuliotajiwa majina yao.
2 – Kuamini Idadi yao; Na idadi yao hakuna anayeijua isipokuwa Allah.
3 – Kuamini Sifa zao kama zilivyokuja katika Qur’ani na hadithi sahihi.
4 – Kuamini Kazi zao.
Usikose makala namba 17 inayofuata in shaa Allah.
Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Imeandaliwa: Tarehe 22 – Rabi’u-Awwal – 1442H ≈ 08 – November – 2020M.
Tembelea website yetu: ⇩⇩ https://www.fawaidusalafiya.net
Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz
Kupata darasa za ndoa jiunge nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/Darasazandoa
Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•