17 – Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya aqida /itikadi kwa vitoto vidogo (chipukizi)

س: ١٧

Swali no. 17:

مَا مَعْنَى الْإِيْمَانِ بِالكُتُبِ؟

Nini maana ya kuamini vitabu?

ج:

Jawabu:

التَّصِدِيْقُ بِهَا.

(Maana yake) ni kuvisadikisha.

سلسلة بطاقات: العقيدة لبراعم الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي.

[ Mtiririko wa vikadi: Itikadi kwa chipukizi (vitoto) vya kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy ]

Maelezo ya Mfasiri:

Mzazi /Mlezi hapa utamuelezea mtoto kwamba Allah ameteremsha vitabu kwa Mitume ili kuwaongoza watu na ni lazima kuviamini na kukubali kuwa vimetoka kwa Allah na miongoni mwa vitabu tumetajiwa majina yao navyo ni Zaburi, Torati, Injili na Quran na vitabu vya Ibrahimu na Musa, na pia tunaamini kila kitabu ambacho Allah amekiteremsha kwa Mtume katika Mitume yake yaani vile ambavyo Allah hakututajia majina yake.

Tanbihi: Vitabu hivi alivyoviteremsha Allah – aliyetukuka – ni maneno yake Allah na si viumbe. Tunapoamini Qur’ani kuwa ni maneno ya Allah ni wajibu baada ya kukiri hilo kuifanyia kazi kwa kuifuata. Ama vitabu vilivyotangulia vyote vimebadilishwa na kupinduliwa na kuongezwa maneno na kupunguzwa na hata yale yaliyobakia sahihi baada ya kuteremshwa Qur’ani tu hukumu yake yameshafutwa kwa maana haifai muislamu kuyafanyia kazi mafundisho hayo. Haifai kwa muislamu kuvimiliki vitabu hivi yaani Injili ambayo kwa sasa wanakiita Biblia ambayo ni mkusanyiko wa Torat, Zaburi, injili ila kwa wanachuoni waliobobea katika Qur’ani na sunnah wanaotaka kubainisha upotevu wa yale yaliyomo humo.

Usikose makala namba 18 inayofuata in shaa Allah.

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Imeandaliwa: Tarehe 23 – Rabi’u-Awwal – 1442H ≈ 09 – November – 2020M.

Tembelea website yetu: ⇩⇩ https://www.fawaidusalafiya.net

Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz

Kupata darasa za ndoa jiunge nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/Darasazandoa

Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *