17- Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya tabia za mtoto wa kiislamu

17- Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya tabia za mtoto wa kiislamu

Makala namba 17:

الْحُبُّ فِي اللّٰهِ:

Kupenda kwa ajili ya Allah:

قَالَ رَسُوْلُ اللَّٰهِ صَلَّى اللّٰهُ عَلَيْهِ وَسَلّمَ

Amesema Mtume – swala na salamu za Allah ziwe juu yake;

أَوْثَقُ عُرَى الإيْمَانِ: الْمُوَالَاةُ فِي اللّهِ،والْمُعَادَاةُ فِي اللَّهِ، والْحُبُّ فِي اللَّهِ، والْبُغْضُ فِي اللَّهِ عزَّوَجَلَّ.

Kishikilio madhubuti cha imani ni: kunusuriana kwa ajili ya Allah na kujenga uadui kwa ajili ya Allah, na kupenda kwa ajili ya Allah na kuchukia kwa ajili ya Allah – aliyeshinda na kutukuka.

صحيح الجامع (٢٥٣٩)

[ سلسلة براعم بينونة أخلاق الطفل المسلم – ١٧ ]

Maelezo:

Mzazi /Mlezi inatakikana umfundishe mwanao kuwa kupendana kwa ajili ya Allah na kunusuriana na kuchukiana na kufanyiana uadui kwa ajili ya Allah ni msingi mkubwa. Muislamu anatakiwa awapende waislamu wote kwa kadri ya imani zao yaani muislamu aliyesimama sawa sawa katika dini na suna huyu anapendwa mia kwa mia, ama muislamu mwenye maovu lakini bado ni muislamu anapendwa kwa kadri ya imani yake na anachukiwa kwa uovu wake, ama watu wa bidaa tunawadhihirishia chuki na kuwabughudhi kimuonekano pamoja na kubakia mapenzi ya moyoni kwa sababu ya uislamu, ama Makafiri na Washirikina hatuwapendi hata kidogo lakini tunawafanyia wema na ihsani kimuonekano kwa wale wasioupiga vita uislamu pamoja na kubakia na bugdha katika nyoyo zetu.

Usikose makala namba 18, in Shaa Allah..

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Imeandaliwa: Tarehe 08/ Jumaadal-aakhir 1442H ≈ 21/ Jan, 2021M.

Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

JIUNGE NASI TELEGRAM KUPATA FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⤵️ https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/Darasazandoa •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *