س: ٢٠
Swali no. 20:
كَيْفَ نُؤْمِنُ بِالرُّسُلِ؟
Vipi tunawaamini Mitume?
ج:
Jawabu:
بالتَّصْدِيْقِ بِهِمْ
(Tunawaamini) kwa kuwasadikisha.
سلسلة بطاقات: العقيدة لبراعم الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي.
[ Mtiririko wa vikadi: Itikadi kwa chipukizi (vitoto) vya kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy ]
Maelezo ya Mfasiri:
Mzazi /Mlezi hapa utamuelezea mtoto kuwa: Kuwaamini Mitume na kuwasadikisha kumekusanya mambo manne (4);
1 – Kuamini kwamba ujumbe waliokuja nao ni kweli unatoka kwa Allah na mwenye kumpinga mmoja tu atakuwa amewapinga wote.
2 – Kuwaamini wale ambao tunayajua majina yao mfano: Muhammad, Ibrahim, Issa, Mussa na Nuhu, swala na salam za Allah ziwe juu yao.
3 – Kusadikisha na kuyakubali yale yaliyoswihi kutoka kwao katika habari zao mbali mbali kuhusu wao.
4 – Kuifanyia kazi sheria ambayo amekuja nayo kwetu sisi Mtume wa mwisho naye ni Muhammad swala na salam za Allah ziwe juu yake.
Usikose makala namba 21 inayofuata in shaa Allah.
Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Imeandaliwa: Tarehe 28 – Rabi’u-Awwal – 1442H ≈ 14 – November – 2020M.
Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
JIUNGE NASI TELEGRAM KUPATA FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⤵️ https://t.me/fawaidussalafiyatz •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•