20- Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya tabia za mtoto wa kiislamu

20- Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya tabia za mtoto wa kiislamu

Makala namba 20:

بِرُّ الْوَالِدَيْنِ:

Kuwatendea wema wazazi wawili:

قَالَ رَسُوْلُ اللَّٰهِ صَلَّى اللّٰهُ عَلَيْهِ وَسَلّمَ:

Amesema Mtume wa Allah – swala na salamu za Allah ziwe juu yake:

رَغِمَ أنْفُ ثُمَّ رَغِمَ أنْفُ ثُمَّ رَغِمَ أنْفُ قيلَ: مَنْ؟ يا رَسولَ اللهِ قالَ: مَن أدْرَكَ أبَوَيْهِ عِنْدَ الكِبَرِ أحَدَهُما أوْ كِلَيْهِما فَلَمْ يَدْخُلِ الجَنَّةَ

Amedhalilika na kufedheheka, kisha amedhalilika na kufedheheka, kisha amedhalilika na kufedheheka,

Kukasemwa: Ni nani (huyo)? ewe Mtume wa Allah! Akasema (akajibu):

Ni yule ambaye amewadiriki (amewawahi) wazazi wake wawili wakati wa uzee wao mmojawapo au wote wawili na akawa hajaingia peponi.

رواه مسلم (٢٥٥١)

[ سلسلة براعم بينونة أخلاق الطفل المسلم – ٢٠ ]

Maelezo:

Mzazi /Mlezi mfahamishe mwanao kuwa kuwafanyia wema wazazi wawili ni sababu katika sababu za kuingia peponi na haswa wanapokuwa watu wazima kwa sababu muda huo wana haja zaidi ya kufanyiwa wema, kwa hiyo kuwafanyia wema kipindi hiki cha utu uzima na udhaifu kwa kuwahudumia na kuwalisha na huduma nyinginezo ni sababu ya kuingia peponi, na mwenye kuzembea katika hilo atapitwa na fursa hii ya kuingia peponi na bila shaka mtu huyu amefadheheka na kudhalilika.

Usikose makala namba 21, in Shaa Allah..

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Imeandaliwa: Tarehe 17/ Jumaadal-aakhir 1442H ≈ 30/ Jan, 2021M. Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

JIUNGE NASI TELEGRAM KUPATA FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⤵️ https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/Darasazandoa •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *