س رقم: ٢٢
Swali no. 22:
مَا هُوَ الإيْمَانُ بِالْيَوْمِ الآخِرِ؟
Ni kupi kuamini siku ya mwisho?
ج:
Jawabu:
هُوَ الإيْمَانُ بِيَوْمِ الْقِيَامَةِ وَالْجَنَّةِ والنّارِ.
Ni kuamini siku ya kiama na pepo na moto.
سلسلة بطاقات: العقيدة لبراعم الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي.
[ Mtiririko wa vikadi: Itikadi kwa chipukizi (vitoto) vya kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy ]
Maelezo ya Mfasiri:
Mzazi /Mlezi hapa utamuelezea Mtoto kuwa: Kuamini siku ya mwisho /siku ya kiama ni kuamini yote yatakayotokea mara tu baada ya kufa na siku ya kiama kama vile moto, pepo, mizani, kuhesabiwa, kuvuka katika siratwa , pepo, moto, n.k
Na kuamini siku ya mwisho kuna daraja mbili (2):
1 – Daraja la imani ya kukata yaani imani ya moja kwa moja isiyokuwa na shaka hata chembe na daraja hili la imani ni lazima kwa maana mwenye shaka na siku hii ya kiama anakuwa kafiri.
2 – Daraja la pili ni imani iliyokita hii ni ile imani ya kuamini siku hii kana kwamba anaiona kwa macho yake na hili ni daraja la juu zaidi kuliko la mwanzo.
Usikose makala namba 23 inayofuata in shaa Allah.
Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Imeandaliwa: Tarehe 01 – Rabi’u-Thaani – 1442H ≈ 16 – November – 2020M.
Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
JIUNGE NASI TELEGRAM KUPATA FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⤵️ https://t.me/fawaidussalafiyatz •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•