س: ٢٣
Swali no. 23:
كَيْفَ نُؤْمِنُ بالْقَدَرِ؟
Vipi tunaamini qadari?
ج:
Jawabu:
بالرِّضَى بِقَضَاءِ اللّٰهِ.
(Tunaamini) kwa kuridhia Makadirio ya Allah.
سلسلة بطاقات: العقيدة لبراعم الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي.
[ Mtiririko wa vikadi: Itikadi kwa chipukizi (vitoto) vya kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy ]
Maelezo ya Mfasiri:
Mzazi /Mlezi hapa utamuelezea mtoto kuwa: Kuamini kadari muradi wake ni kuamini ukadiriaji wa Allah kwa vitu vyote, yaani Allah kujua matukio (yote) na kuyaandika na kutaka (yatokee) na kuyaumba.
Ufafanuzi: Allah anajua kila kitu yaliyotokea, yatakayotokea, yasiyotokea n.k . Kila kinachotokea Allah – aliyetukuka – amekiandika. Kila kinachotokea Allah ametaka kitokee kwa hekima maalumu tuijue au tusiijue. Na vyote vinavyotokea vimeumbwa na Allah. Mja/mwanadamu ana hiari na matakwa lakini hawezi kutaka kitu mpaka Allah atake, lakini mja ndiye mfanyaji hakika na mja hajui lile alilokadiriwa mpaka litakapotokea.
Usikose makala namba 24 inayofuata in shaa Allah.
Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Imeandaliwa: Tarehe 03 – Rabi’u-Thaani – 1442H ≈ 16 – November – 2020M.
Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
JIUNGE NASI TELEGRAM KUPATA FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⤵️ https://t.me/fawaidussalafiyatz •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•