س:
Swali no 24:
مَا هُوَ حَقُّ الصَّحَابَةِ؟
Ni ipi haki ya Maswahaba?
ج:
Jawabu:
مَحَبَّتُهُمْ والاقْتِدَاءُ بِهِمْ .
(Haki ya Maswahaba) ni kuwapenda na kuwaiga.
سلسلة بطاقات: العقيدة لبراعم الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي.
[ Mtiririko wa vikadi: Itikadi kwa chipukizi (vitoto) vya kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy ]
Maelezo ya Mfasiri:
Mzazi /Mlezi hapa utamuelezea mtoto kuwa: Uislamu ni kama nyumba na maswahaba ndio mlango, njia sahihi ya kuingia ndani ni kupitia mlangoni basi ndio hivi hivi njia sahihi ya kuufahamu uislamu ni kushikamana na maswahaba ambao ni wanafunzi wa Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie -, kwa sababu wao ndio walioupokea uislamu kutoka kwa Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – wao ndio walio pokea qur’ani na hadithi /suna, kuwapenda maswahaba ni katika dini na ni wajibu /lazima na kuwachukia maswahaba ni unafiki.
Maswahaba wapo wengi sana lakini wabora wao zaidi ni wanne ambao walikuwa viongozi baada ya Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie:
1 – Abuu Bakr Sswiddiiq – Allah amridhi – kiongozi wa kwanza baada ya Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie –
2 – Umar bin l-Khattwaab – Allah amridhie –
3 – Utman bin ‘Affaan – Allah amridhie –
4 – Aliy bin Abii Twaalib – Allah amridhie –
Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Imeandaliwa: Tarehe 04 – Rabi’u-Thaani – 1442H ≈ 19 – November – 2020M.
Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
JIUNGE NASI TELEGRAM KUPATA FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⤵️ https://t.me/fawaidussalafiyatz •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•