Makala namba : 2
قال تعالى :
Amesema (Allah) aliyetukuka-:
﴿ إِذْ قَالَ يُوسُفُ لِأَبِيهِ يَا أَبَتِ إِنِّي رَأَيْتُ أَحَدَ عَشَرَ كَوْكَبًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ رَأَيْتُهُمْ لِي سَاجِدِينَ } ( ٤ )
Kumbuka Yusuf pindi alipo mwambia baba yake : Ewe baba yangu !bila shaka mimi nimeona (ktk ndoto) nyota kumi na moja ,na jua na mwezi.Nimeona zikinisujudia .
﴿ قَالَ يَا بُنَيَّ لَا تَقْصُصْ رُؤْيَاكَ عَلَى إِخْوَتِكَ فَيَكِيدُوا لَكَ كَيْدًا إِنَّ الشَّيْطَانَ لِلْإِنْسَانِ عَدُوٌّ مُبِينٌ } (٥)
(Baba) akasema: Ewe kitoto changu !Usiwasimulie ndugu zako ndoto yako ,wasije wakakufanyia vitimbi vikubwa .Bila shaka Shetani ni adui aliye wazi kwa mwanadamu .
Maelezo :
Hapa ndipo kunapoanza kisa cha Yusuf -Amani iwe juu yake – pindi Yusuf alipoona ndotoni nyota kumi na moja na jua na mwezi vikimsujudia na kumnyenyekea ,na ndoto za mitume ni haki na kweli.
Lakini baba wa Yusuf (nabii Yaqub ) -amani iwe juu yake- alijua kuwa hii ndoto ina ishara kubwa na huyu mwanaye atakuwa mtu mkubwa, na alimkataza mwanaye kuwasimulia ndoto hii ndugu zake kwa kuhofia husuda wanayoweza kumfanyia kwa kumuangamiza kutokana na vishawishi vya shetani kwao ,kwa sababu watajua kuwa maana ya ndoto hii ni kuwa zile nyota ni wao ,jua ni baba yao na mwezi ni mama yao ,kwa maana watajua kuwa maana ya ndoto hii ni kuwa Yusuf -amani iwe juu yake- atakuwa mtu mkubwa .
Na hii ni kawaida ya watu humhusudu yule ambaye ameneemeshwa neema ambayo wao hawajapewa .Na pia tunajifunza kuwa si kila unapopata neema fulani unamsimulia kila mtu ,kwa maana kama kuna maslahi ya kuficha baadhi ya neema basi ifiche ,kama ilivyokuja katika hadith :
” استعينوا على إنجاح الحوائج بالكتمان فإن كل ذي نعمة محسود “
” Takeni msaada juu ya kufaulu haja (zenu) kwa kuficha bila shaka kila mwenye neema huhusudiwa ”
صحيح الجامع برقم ٩٤٣.
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Ramadhani 14, 1442H ≈ April 26, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•