6- Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya tabia za mtoto wa kiislamu

06- Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya tabia za mtoto wa kiislamu

Makala namba 6:

الرَّحْمَةُ:

Huruma:

قَالَ رَسُوْلُ اللَّٰهِ صَلَى اللّٰهِ عَلَىيْهِ وسَلّمَ

Amesema Mtume was Allah swala na salamu za Allah ziwe juu yake:

تَرَى المُؤْمِنِينَ فِي تَرَاحُمِهِمْ وَتَوَادِّهِمْ وَتَعَاطُفِهِمْ، كَمَثَلِ الجَسَدِ، إِذَا اشْتَكَى عُضْوًا تَدَاعَى لَهُ سَائِرُ جَسَدِهِ بِالسَّهَرِ وَالحُمَّى

رواه البخاري رقم الحديث (٦٠١١)

Ukiwaona waumini katika kuhurumiana kwao na kupendana kwao na kuafikiana kwao (kusaidiana) ni kama mfano wa mwili (mmoja) pindi kitakapougua kiungo kimoja huitana viungo vya mwili wake wote kwa kukesha na (maumivu ya) homa. Ameipokea Al-bukhariy (hadithi) namba 6011

[ سلسلة براعم بينونة أخلاق الطفل المسلم – ٦ ]

Maelezo:

Mzazi /Mlezi inatikana umfundishe mwanao kuwa waislamu huoneana huruma kwa ule undugu wa kiislamu, na vile vile huyafanya yale ambayo ni sababu ya kuleta mapenzi baina yao kama kutembeleana, na kupeana zawadi, na pia husaidiana na kufungamana mfano wao ni kama mwili mmoja kama kiungo kimoja kitaugua basi mwili mzima utakesha kwa maumivu pamoja na viungo vyote, hivi ndivyo waislamu wanatakiwa wawe. Usikose makala namba 7, in Shaa Allah..

Mfasiri: fawaidusalafiya.net Imeandaliwa: Tarehe 12/ Jumaadal-ulaa, 1442H ≈ 27/December, 2020M.

Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

JIUNGE NASI TELEGRAM KUPATA FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⤵️ https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/Darasazandoa •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *