8- Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya tabia za mtoto wa kislamu

08- Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya tabia za mtoto wa kiislamu

Makala namba 8:

الصّلَاةُ عَلَى النّبِيّ صَلَّى اللّٰهِ عَلَىيْهِ وسَلّمَ:

Kumswalia Mtume – swala na salamu za Allah ziwe juu yake:

قَالَ رَسُوْلُ اللَّٰهِ صَلَّى اللّٰهِ عَلَىيْهِ وسَلّمَ

Amesema Mtume – swala na salamu za Allah ziwe juu yake:

” مَن صَلَّى عَلَيَّ وَاحِدَةً، صَلَّى اللَّٰهُ عَلَيْهِ بِهَا عَشَرًا ” رواه مسلم ( ٤٠٨)

” Mwenye kuniswalia mimi mara moja, Allah atamswalia mara kumi kutokana na swala hiyo ”

Ameipokea Muslim namba ya hadithi ni (408)

Maelezo:

Mzazi /Mlezi inatakikana umuelezee mwanao maana ya kumswalia Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – na ubora wa hilo: Maana ya kumswalia Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – ni kumuomba Allah azidi kuunyanyua utajo wa Mtume wake na kumsifu na kumweka karibu. Kumswalia Mtume ni ibada yenye ujira mkubwa kama vile ilivyokuja katika hadithi hii tuliyokuwa nayo kwamba: ukimswalia mara moja basi Allah anakutaja (anakurehemu) huko mbinguni mara kumi, na anakunyanyua daraja kumi, na unaandikiwa mema kumi, na unafutiwa madhambi kumi, na pia katika watu bora siku ya kiama ni wale wenye kukithirisha kumswalia Mtume – swala salamu za Allah zimfikie – na pia ni sababu ya kuwa karibu na Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – Na vile vile mtu bakhili ni yule ambaye Mtume – swala na salamu zimfikie – anapotajwa akawa hamswalii, na huyu ni mtu aliyepata hasara. Na haswa inatakikana kukithirisha kumswalia Mtume – swala na salamu zimfikie – sana siku ya ijumaa. Ajiepushe na kumswalia Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – kwa mitindo ya kizushi ambayo haikuthibiti katika sheria.

Usikose makala namba 9, in Shaa Allah.. Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Imeandaliwa: Tarehe 17/ Jumaadal-ulaa, 1442H ≈ 01/ Jan, 2021M.

Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

JIUNGE NASI TELEGRAM KUPATA FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⤵️ https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/Darasazandoa •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *