UMUHIMU WA KUDUMU NA NYIRADI .

‏قال الشيخ العلامة ⁧ ابن_باز⁩ رحمه الله :

Amesema sheikh mwanachuoni mkubwa ibn Baaz-Allah amrahamu-:

‏” المعوذتان صباحاً ومساءً ثلاث مرات ،

‏من أسباب السلامة من السحر وغيره “

” Suratul-falaq na suratu-Nnas asubuhi na jioni mara tatu ni miongoni mwa sababu za  kusalimika na uchawi na mengineyo ”

‏{📔فتاوى نور على الدرب – ٢٩٥/٣ }

Maelezo:

Kudumu na nyiradi za asubuhi na jioni ni katika sababu za kukingwa na uchawi,kijicho,kuumwa na vidudu ,na shari nyinginezo .

KINACHOPOROMOSHA MEMA YOTE !

قـ✑ـال  ابن تيميـة – رحمــه الله – :

Amesema ibn Taimiyyah-Allah amrahamu-:

 لا يُحبِطُ جميع الحسنات إلا الكفر ،

كما لا يُحبِطُ جميع السيئات إلا التوبة .

(Hakuna kinachoporomosha mema yote isipokuwa ukafiri /ushirikina, kama (ilivyokuwa) hakuna kinachoporomosha madhambi yote isipokuwa toba ”

📚 مجموع الفتاوىٰ (٣٢٢/١٠)

Maelezo:

Muislamu aliyemshirikisha Allah ushirikina mkubwa basi ajue kuwa mema yake yote yameporomoka na akifa bila ya toba atakaa motoni milele, kama ilivyokuwa kafiri akiingia ktk uislamu anakuwa kama amezaliwa bali mabaya yake yanageuzwa mema .

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *