Je, inafaa Muislamu kusoma nyota na kujua mambo ya baadae?

Anasema muulizaji:

Je, inaruhusiwa kwa muislamu kusoma nyota na kupata faida (kujua) mambo ya baadae kutoka katika hizo (nyota), bila ya kuitakidi kufaa kwake?

Jawabu (la Sheikh):

Tunamuomba Allah afya, hili halifai, haifai kuamini nyota, sayari juu ya matukio (mbalimbali), huu ni unajimu: { Mwenye kujifundisha sehemu ya elimu ya nyota bila shaka amejifundisha sehemu ya ushirikina, kila anapozidi kujifundisha elimu ya nyota huzidi kujifundisha ushirikina }

Nyota ameziumba Allah kwa ajili ya (vitu) vitatu:

1 – Pambo la mbingu.

2 – Na vimondo vya kuwapiga mashetani.

3 – Na alama (ambazo) hupatikana uongofu (wa kufahamu maeneo) katika giza la bara na baharini.

Basi yeyote mwenye kupindua (kudai) kwa tafsiri isiyokuwa hiyo, bila shaka amedanganya na amepoteza sehemu (ya umri wake). Ndio, amejifedhehesha na amefanya ushirikina na amepoteza sehemu ya (umri) wake.

Mjibuji swali: Sheikh Swaalih Fauzaan Al-fauzaan

Mfasiri: fawaidusalafiya.net Kiunganishi cha sauti ya Sheikh: https://youtu.be/QB7YW667BEk

Imeandaliwa: Tarehe 07 – Safar – 1442H ≈ 24 – September – 2020M.

Kiunganishi: https://t.me/fawaidussalafiyatz

Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz

Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz

Muhimu: Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *