قال تعالى
Amesema (Allah) – aliyetukuka:
وما تدري نفس بأي أرض تموت
{ Na wala nafsi haijui itakufa katika ardhi gani }
قال شيخنا ابن عثيمين رحمه الله
Amesema Sheikh wetu ibn ‘Uthaimin – Allah amrahamu-:
لا تدري متى تموت ولا بأي أرض تموت. فإذا كنت كذلك فاقصر الأمل لا تمد الأمل طويلا، لا تقل أنا شاب وسوف أبقى زمانا طويلا فكم من شاب مات في شبابه وكم من شيخ عُمِّر
(Nafsi) haifahamu lini itakufa na wala (haifahamu) itakufa ardhi gani. Basi ukiwa upo hivi, punguza matarajio na wala usiyarefushe matarajio (yakawa) marefu, wala usiseme mimi ni kijana nitabakia muda mrefu, basi ni vijana wangapi wamefariki katika ujana wao na wazee wangapi wamepewa umri mrefu.
شرح رياض الصالحين ٤٤٢/٢
Maelezo:
Maana yake ni kuwa kuna vijana wengi ambao watu walikuwa wakitaraji kuwa wataishi muda mrefu lakini ghafla wakafariki hali ya kuwa ni wabichi katika ujana wao na nguvu zao, na pia kuna wazee wengi ambao watu walikuwa wakiwangojea siku yoyote watafariki lakini wakaishi muda mrefu! Tujiandae kifo huja muda wowote.
Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Imeandaliwa: Tarehe 09 – Safar – 1442H ≈ 26 – September – 2020M.
Kiunganishi: https://t.me/fawaidussalafiyatz
Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz
Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz
Muhimu: Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•