ذكر الاستيقاظ من النوم
Nyiradi ya kuamka kutoka usingizini
الحَمْدُ لله الذِي أحْيَانا بَعْدَ مَا أمَاتَنَا وإلَيْهِ النَشُور
” Sifa zote njema ni za Allah ambaye ametufufua baada ya kutufisha na kwake ndiyo kufufuliwa ”
البخاري مع الفتح 11/ 113 ومسلم 4/ 2083
Maelezo: Usingizi ni ndugu wa kifo, yaani usingizi ni sehemu ya kifo kwa sababu mtu anapolala anakosa hisia na hili limethibiti kutoka kwa Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie -:
روا الطبراني من جابر بن عبد الله سئل نبي الله فقيل
Amepokea Attwabaraniy katika hadith ya Jabir bin Abdillah – aliulizwa Nabii wa Allah:
يا رسول الله أينام أهل الجنة فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم
Ewe Mjumbe wa Allah; Je watu wa peponi wana lala? basi akasema Mtume wa Allah – swala na salamu za Allah zimfikie -:
النوم أخو الموت وأهل الجنة لا ينامون
” Usingizi ni ndugu wa kifo na watu wa peponi hawalali ”
Uchanganuzi:
Watu wa peponi hawachoki na wala hawaumwi kwa hiyo hawana haja ya kulala ili wapumzike, na pia usingizi utawafanya wapitiwe na muda bila ya kufurahi na kustarehe. Allah – aliyetukuka – amesema – akielezea usingizi kuwa ni katika kifo:
اللَّهُ يَتَوَفَّى الْأَنفُسَ حِينَ مَوْتِهَا وَالَّتِي لَمْ تَمُتْ فِي مَنَامِهَا ۖ فَيُمْسِكُ الَّتِي قَضَىٰ عَلَيْهَا الْمَوْتَ وَيُرْسِلُ الْأُخْرَىٰ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ
{ Allah huzichukua roho zinapo kufa. Na zile zisizokufa wakati wa kulala kwake, huzizuia zile zilizohukumiwa kufa, na huziachia nyingine mpaka ufike muda wake uliowekwa (wa kufa).Hakika katika hayo bila shaka kuna alama kwa watu wanaofikiri }
الزمر:٤٢
Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Imeandaliwa: Tarehe 13 – Safar – 1442H ≈ 30 – September – 2020M.
Kiunganishi: https://t.me/fawaidussalafiyatz
Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz
Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz
Muhimu: Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•