002 – Nyiradi inayosomwa pindi mtu atakapozinduka usingizini au anapoamka

لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ لهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ سُبْحَانَ اللَّهِ وَالحَمْدُ للَّهِ وَلاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَاللَّهُ أَكبَرُ وَلاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللَّهِ الْعَلِيِّ الْعَظِيمِ رَبِّ اغْفرْ لِي

{ Hakuna muabudiwa anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah pekee hana mshirika, ufalme ni wa kwake tu na sifa zote njema ni zake pekee na yeye juu ya kila kitu ni muweza, utakasifu ni wake na sifa zote njema ni zake na hakuna muabudiwa anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah na Allah ni mkubwa kuliko vyote na hakuna ujanja wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allah aliyekuwa juu na mtukufu, (ewe) Allah nisamehe }.

ثم قال صلى الله عليه وسلم

Kisha akasema – swala na salamu za Allah zimfikie:

من قال ذلك غُفِرَ له فإن دعا استجيب له فإن قام فتوضأ ثم صلى قُبلت صلاته

Mwenye kuyasema (maneno) hayo atasamehewa (madhambi) na kama ataomba (dua) atajibiwa na kama atasimama akatawadha kisha akaswali swala yake itakubaliwa.

البخاري مع الفتح 3/ 39 برقم 1154 وغيره واللفظ لابن ماجه انظر صحيح ابن ماجه 2/335

Maelezo: Hii ni nyiradi ambayo anaisoma muislamu pindi anapozinduka usingizini usiku au anapoamka na fadhila za kutamka maneno hayo ni kusamehewa madhambi na kujibiwa dua kama ataomba dua na kukubaliwa swala yake kama ataswali.

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Imeandaliwa: Tarehe 15 – Safar – 1442H ≈ 02 – October – 2020M.

Kiunganishi: https://t.me/fawaidussalafiyatz

Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz

Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz

Muhimu: Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *