06 – Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya aqida /itikadi kwa vitoto vidogo (chipukizi)

س: ٦

Swali no. 6:

مَا أَعْظَمُ أَرْكَانُ الْإِسْلَامِ؟

Ni ipi nguzo kubwa zaidi ya Uislamu?

ج:

Jawabu:

شهادةُ أَنْ لَا إِلٰهَ إِلَا اللهُ.

Ni kushuhudia kwamba hakuna muabudiwa anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah.

سلسلة بطاقات: العقيدة لبراعم الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي

[ Mtiririko wa vikadi: Itikadi kwa chipukizi (vitoto) vya kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy ]

Maelezo ya Mfasiri:

Mzazi /Mlezi hapa utamuelezea mtoto hii ni nguzo kubwa zaidi na ndio tamko ambalo mtu hawi muislamu ila kwa tamko hili, Na tamko hili lina nguzo mbili;

1 – Ukanushaji unaoenea kwa kila kinachoabudiwa kinyume na Allah kama: Masanamu, makaburi, mizimu n.k.

2 – Uthibitishaji haswa: yaani unathibitisha ibada kwa Allah tu peke yake. Na tamko hili linaambatana na kushuhudia utume wa Muhammad – swala na salamu za Allah zimfikie – kwa maana mwenye kudai kuwa anampwekesha Allah lakini akakataa utume wa Muhammad huyo si muislamu, kama ilivyokuwa mwenye kumuamini Mtume lakini akawa hajampwekesha Allah hawi muislamu pia.

Usikose makala namba 07 inayofuata in shaa Allah.

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Imeandaliwa: Tarehe 04 – Rabi’u-Awwal – 1442H ≈ 21 – October – 2020M.

Tembelea website yetu: ⇩⇩ https://www.fawaidusalafiya.net

Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz

Kupata darasa za ndoa jiunge nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/Darasazandoa

Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *