07 – Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya aqida /itikadi kwa vitoto vidogo (chipukizi)

س: ٧

Swali no. 7:

ماَ مَعْنَى لَا إِلٰهَ إِلَّا اللّٰهُ؟

Nini maana ya hapana Muabudiwa apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah?

ج:

Jawabu:

لَا مَعْبُودَ حقٌّ إلَّا اللَّهُ

(Maana yake) Hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Allah.

سلسلة بطاقات: العقيدة لبراعم الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي

[ Mtiririko wa vikadi: Itikadi kwa chipukizi (vitoto) vya kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy ]

Maelezo ya Mfasiri:

Mzazi /Mlezi hapa utamuelezea mtoto maana sahihi ya tamko hili yaani hakuna muabudiwa anayebudiwa kwa haki isipokuwa Allah, kwa maana vinavyo abudiwa kwa dhulma na kuchupa mipaka ni vingi mno, mfano kuna watu wanaabudia Makaburi, Mitume kama vile Isa bin Mariam – Amani iwe juu yake -, Mashetani, Masanamu n.k, Lakini anayeabudiwa kwa haki ni Allah peke yake, ukijua hili utajua kuwa ni makosa makubwa kutafsiri tamko hili kwa kusema:

” Hakuna anayeabudiwa (Mungu) isipokuwa Allah! ”

Kwa sababu tafsiri hii inaashiria kuwa miungu yote inayoabudiwa ni Allah yaani kila kinachoabudiwa ni Allah. Kwa hiyo ni lazima uweke neno ” kwa haki ” kwa maana vinavyoabudiwa kwa dhulma ni vingi lakini anayeabudiwa kwa haki ni Allah peke yake. Usikose makala namba 08 inayofuata in shaa Allah.

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Imeandaliwa: Tarehe 05 – Rabi’u-Awwal – 1442H ≈ 22 – October – 2020M.

Tembelea website yetu: ⇩⇩ https://www.fawaidusalafiya.net

Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz

Kupata darasa za ndoa jiunge nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/Darasazandoa

Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *