003 – Adhkari /nyiradi za asubihi (no. 01)

☞ Kusoma Ayatul-kursiy asubihi na jioni.

أَعُوذُ بِاللَّهِ مِنَ الشَّيطَانِ الرَّجِيمِ

Nakimbilia/najikinga kwa Allah kutokana na shetani aliyefukuzwa katika rehema za Allah.

اللَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ مَنْ ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِنْدَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ

{ Allah – hapana muabudiwa anayestahiki kuabudiwa isipokuwa yeye aliye hai aliyesimama kwa dhati yake/Msimamiaji mambo yote milele. Hashikwi na kusinzia wala usingizi. Ni vyake pekee vyote vilivyomo mbinguni na ardhini. Hakuna yeyote anayeweza kuombea mbele bila ya idhini yake (kwa utukufu wake), Anayajua yote yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao (yaliyopita); Na wala wao hawajui chochote katika elimu yale anayoyajua ila kwa yale anayoyataka. Kimezunguka kiti chake mbinguni na ardhini; na wala havimtii uzito kuvihifadhi viwili hivyo (mbingu na ardhi na vilivyomo). Na yeye ndiye aliyejuu na Mkubwa }

آية الكرسي

Maelezo ya Mfasiri:

Katika ubora wa aya hii tukufu zaidi katika qurani ni maneno aliyoyazungumza Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie:

من قالها حين يصبح أُجير من الجن حتى يمسي، ومن قالها حين يمسي أُجير منهم حتى يصبح

{ Mwenye kuisoma hiyo (Ayatul-Kursiy) pindi anapoingia asubuhi atakingwa na majini mpaka jioni na mwenye kuisoma pindi anapoingia jioni atakingwa na majini mpaka asubuhi }

صحيح الترغيب ٦٦٢

Vile vile katika ubora wa kuisoma Ayatul-kursiy ni kwamba mwenye kudumu na kuisoma aya hii kila baada ya swala tano hakuna kitakachomzuia kuingia peponi isipokuwa kifo kama alivyosema Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie-, vile vile amesema – Mwenye kuisoma usiku kabla ya kulala ataletewa mlinzi mpaka asubuhi.

Ufafanuzi:

Al-kursiy: ipo chini ya arshi ambayo ni sehemu ya nyayo mbili za Allah – aliyetukuka – zinazonasibiana na utukufu wake na ukamilifu wake na wala hazifanani na nyayo za yeyote katika viumbe. Na hiyo kursiy ni kubwa kuliko mbingu saba na ardhi saba yaani mbingu saba na ardhi saba vyote vinaingia katika hii kursiy (Kiti) na pia Arshi ambayo Allah – aliyetukuka – yupo juu yake ni kiumbe kikubwa mno kuliko viumbe vyote.

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Imeandaliwa: Tarehe 07 – Rabi’u-Awwal – 1442H ≈ 24 – October – 2020M.

Tembelea website yetu: ⇩⇩ https://www.fawaidusalafiya.net

Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz

Kupata darasa za ndoa jiunge nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/Darasazandoa

Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *