09 – Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya aqida /itikadi kwa vitoto vidogo (chipukizi)

س: ٩

Swali no. 9:

مَا مَعْنَى: اللٌٰهُ إِلٰهُنَا؟

Nini maana ya Allah ndiye Muabudiwa “Mungu” wetu?

ج:

Jawabu:

مَعْبُوْدُنَا وَحْدَهُ

(Maana yake): Ni muabudiwa wetu pekee.

سلسلة بطاقات: العقيدة لبراعم الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي

[ Mtiririko wa vikadi: Itikadi kwa chipukizi (vitoto) vya kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy ]

Maelezo ya Mfasiri:

Mzazi /Mlezi hapa utamuelezea mtoto Maana ya Al-ilahu “Mungu” ni Muabudiwa yaani unaposema: “Hakuna mungu anayeabudiwa kwa haki isipokuwa Allah ” Unakusudia kuwa: Hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Allah na wala haina maana hakuna muumbaji isipokuwa Allah. Maelezo haya ya kusema: Hakuna muumbaji isipokuwa Allah ni sahihi, lakini si maana sahihi ya tamko “Al-ilaah” (Mungu) bali maana yake sahihi ni muabudiwa. Kwa hiyo maana sahihi ya tamko la tauhidi itakuwa: Hakuna muabudiwa (Mungu) anayeabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, kwa sababu Mitume hawakutumwa kuja kuwafahamisha watu kuwa muumbaji ni nani kwa hakika jambo hili hakuna anayelipinga katika wanadamu kwamba muumbaji ni Allah ila ni nadra mno, lakini ulinganiaji wa Mitume ulikuwa katika kuwaelekeza watu katika kumuamini Muabudiwa mmoja na kumuabudia yeye pekee.

Usikose makala namba 10 inayofuata in shaa Allah.

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Imeandaliwa: Tarehe 09 – Rabi’u-Awwal – 1442H ≈ 26 – October – 2020M.

Tembelea website yetu: ⇩⇩ https://www.fawaidusalafiya.net

Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz

Kupata darasa za ndoa jiunge nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/Darasazandoa

Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *