10 – Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya aqida /itikadi kwa vitoto vidogo (chipukizi)

س: ١٠

Swali no. 10:

كَْيفَ عَرَفْتَ اللّٰهَ؟

Vipi umemtambua Allah?

ج:

Jawabu:

بأسِمَاىٔهِ و صِفَاتِهِ وَ بِمَخْلُوْقَاتِهِ

(Nimemtambua Allah) kwa majina yake na sifa zake na kwa viumbe vyake.

سلسلة بطاقات: العقيدة لبراعم الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي.

[ Mtiririko wa vikadi: Itikadi kwa chipukizi (vitoto) vya kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy ]

Maelezo ya Mfasiri:

Hapa Mzazi /Mlezi unamtajia mtoto baadhi ya majina ya Allah kama vile الرزاق (Arrazzaaq) maana ni mwenye kuruzuku kila kiumbe unachokiona na usichokiona vyote vinaruzukiwa na Allah kwa hiyo katika sifa zake Allah ni kuruzuku,

Pia miongoni mwa majina yake (السميع) Mwenye kusikia, kwa maana Allah – aliyetukuka – anasikia kila kitu hakuna kinachofichikana kwake sawa sawa yazungumzwe kwa siri au kwa wazi, kwa hiyo katika sifa zake Allah – aliyetukuka – ni kusikia, majina haya na sifa hizi za Allah hayafanani na yeyote lakini tunamthibitishia kwa namna inayonasibiana na utukufu wake. Katika alama zinazojulisha kuwepo kwa Allah mmoja anayestahiki kuabudiwa ni alama ambazo Allah ameziweka na hizi alama zimegawanyika sehemu mbili:

1 – Alama za kisheria ambazo ni vitabu vyake alivyowashushia Mitume – amani iwafikie – kama Torat, Zabur, Injil na Qur’ani na vinginevyo ambavyo Allah anavijua.

2 – Na kuna alama ya pili ambayo ni viumbe alivyoviumba na kila kiumbe kimeumbwa na Allah, na katika viumbe vikubwa tunavyoviona ni usiku, mchana, jua na Mwezi mpangilio wa viumbe hivi na nidhamu yake ni ishara tosha ya kuwepo Allah mmoja.

Usikose makala namba 11 inayofuata in shaa Allah.

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Imeandaliwa: Tarehe 10 – Rabi’u-Awwal – 1442H ≈ 27 – October – 2020M.

Tembelea website yetu: ⇩⇩ https://www.fawaidusalafiya.net

Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz

Kupata darasa za ndoa jiunge nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/Darasazandoa

Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *