21 – Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya aqida /itikadi kwa vitoto vidogo (chipukizi)

س رقم: ٢١

Swali no. 21:

مَاذَا فِي الْقَبْرِ؟

Kuna nini ndani ya kaburi?

ج:

Jawabu:

نَعِيْمٌ أَوْ عَذَابٌ.

(Kuna) neema au adhabu.

سلسلة بطاقات: العقيدة لبراعم الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي.

[ Mtiririko wa vikadi: Itikadi kwa chipukizi (vitoto) vya kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy ]

Maelezo ya Mfasiri:

Mzazi /Mlezi hapa utamuelezea mtoto kuwa: Kaburi ni mwanzo wa safari ya akhera na maisha ya kaburini ni maisha ya kusubiri siku ya malipo na ni wajibu kuamini yote tuliyoelezwa na Allah na Mtume wake yaani yale yatakayomtokea kila mtu katika kaburi kwa sababu ndani ya kaburi kuna neema kwa watu wema na adhabu kwa waislamu waovu kwa kadri ya uovu wao na makafiri /washirikina wataadhibiwa milele mpaka kiama na kaburini kuna maswali ambayo kila mtu ataulizwa nayo ni: Ni nani Muabudiwa wako? Ni ipi dini yako? Ni nani nabii wako? Maswali hatoweza kujibu isipokuwa yule aliyeishi katika dunia kwa kumpwekesha Allah na kujiepusha na ushirikina na akamfahamu Allah na kumuamini na akaufahamu uislamu na akalazimiana nao.

Usikose makala namba 22 inayofuata in shaa Allah.

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Imeandaliwa: Tarehe 28 – Rabi’u-Awwal – 1442H ≈ 14 – November – 2020M.

Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

JIUNGE NASI TELEGRAM KUPATA FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⤵️ https://t.me/fawaidussalafiyatz •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *