https://www.fawaidusalafiya.net
سلسلة أحكام الجنائز.
MLOLONGO (MFULULIZO) WA HUKUMU ZA MAITI (NO. 33)
☞ NAMNA YA KUSWALIA JENEZA (MAITI)
Makala namba 02:
Ataleta takbira nne na atanyanyua mikono pamoja na kila takbira, na hizi takbira ni nguzo na baadhi ya wanachuoni wa fiqih wanaizingatia nguzo ni takbira ya kufungulia swala tu na nyingine ni suna, na dalili ya hizi takbira:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ أَنَّ النَّبِيَّ ﷺ نَعَى النَّجَاشِيَّ فِي الْيَوْمِ الَّذِي مَاتَ فِيهِ وَخَرَجَ بِهِمْ إلَى الْمُصَلَّى، فَصَفَّ بِهِمْ وَكَبَّرَ عَلَيْهِ أَرْبَعَ تَكْبِيرَاتٍ.
Kutoka kwa Abu Hurairah – Allah amridhie – kwamba Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – alitoa taarifa ya kifo cha Annajash katika siku ambayo aliyofariki na akaenda nao (maswahaba) sehemu ya kuswalia (maiti) akawapanga mstari na akaleta takbira nne.
رَوَاهُ الْجَمَاعَةُ
Na kumethibiti katika hilo hadithi nyingi kutoka kwa Mtume – swala na salamu zimfikie – alileta takbira nne, isipokuwa inaruhusiwa muda mwingine kuleta takbira tano au sita mpaka tisa kwa sababu ya kuthibiti kwa hilo kutoka kwa maswahaba na hizi wanachuoni wanaziita ni tofauti ya aina yaani idadi zote ni sawa na haki isipokuwa mara nyingi inatakiwa ziletwe takbira nne na akizidisha mara moja moja si mbaya ili watu wajue kuwa ni suna, lakini kama watu wamezoea takbira nne usizidishe ila baada ya kuwafundisha na pia uwe ni katika watu wanaoaminiwa na kukubalika mahali husika. Baada ya takbira ya kwanza atasoma suratul-faatiha hii ni kauli ya madhehebu manne, ama kusoma sura nyingine baada ya al-faatiha hayo ni madhehebu ya baadhi ya wanachuoni wa kishafi na Mahanabila kwa sababu ya riwaya ya imamu Annasaiy, na huu ndio msimamo wa Sheikh Al-albaaniy – Allah amrahamu – na pia Sheikh ibn Baaz – Allah amrahamu – ama kutosheka na Al-fatiha ni vizuri kwa sababu swala ya jeneza imejengeka kwa kuwepesishwa na kama ukisoma sura basi soma sura fupi kama Al-ikhlaswi n.k,
عن طلحة بن عبدالله بن عوف، قال:
Kutoka kwa Twal-hah bin Abdillah bin ‘Auf amesema:
صَلَّيتُ خلف ابن عباس – رضي الله عنهما – على جنازة فقرَأ بفاتحة الكتاب وقال:
Niliswalia jeneza fulani nikiwa nyuma ya ibn Abbas – Allah amridhie yeye na baba yake – basi akasoma suratul-faatiha na akasema:
{ لتَعلموا أنه من السُّنة }
{ ili mjue kuwa huo ni mwenendo wa Mtume }
البخاري ١٣٣٥ وغيره
Na kusoma al-fatiha ni nguzo katika swala ya jeneza na anatakiwa mtu asome kwa siri, ama ibn Abbas – Allah amridhie – alidhihirisha ili awafundishe watu kama mwenyewe alivyosema. Itaendelea in shaa Allah,
usikose makala namba 03.
Mfasiri: fawaidusalafiya.net Imeandaliwa: Tarehe 09 – Rabi’ul – aakhir ≈ 24 – November – 2020M. Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
JIUNGE NASI TELEGRAM UPATE FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⤵️ https://t.me/fawaidussalafiyatz •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•