Namna ya kuswalia jeneza (maiti) [ No. 04 ]

https://www.fawaidusalafiya.net

سلسلة أحكام الجنائز.

MLOLONGO (MFULULIZO) WA HUKUMU ZA MAITI (NO. 35)

☞ NAMNA YA KUSWALIA JENEZA (MAITI)

Makala namba 04:

ثم يُكبر التكبيرة الثالثة و يدعو للميِّت، ويُخلص له الدعاء كما ثبت في السنة,

Kisha ataleta takbira ya tatu na atamuombea dua maiti na atamhusishia dua maiti kama ilivyothibiti katika hadithi, Atamuombea maiti dua yoyote iliyokusanya kumtakia msamaha, au kufutiwa madhambi, lakini akisoma dua iliyokuja katika suna ni bora zaidi, na katika dua ambazo Mtume – swala na salamu za Allah alikuwa akizisoma ni hii:

Dua namba 01

اللَّهُمَّ اغْفِرْ لَهُ وَارْحَمْهُ وَعَافِهِ وَاعْفُ عَنْهُ، وَأَكْرِمْ نُزُلَهُ، وَوَسِّعْ مُدْخَلَهُ، وَاغْسِلْهُ بِالْمَاءِ وَالثَّلْجِ وَالْبَرَدِ، وَنَقِّهِ مِنْ الْخَطَايَا كَمَا نَقَّيْتَ الثَّوْبَ الْأَبْيَضَ مِنْ الدَّنَسِ، وَأَبْدِلْهُ دَارًا خَيْرًا مِنْ دَارِهِ، وَأَهْلًا خَيْرًا مِنْ أَهْلِهِ، وَزَوْجًا خَيْرًا مِنْ زَوْجِهِ، وَأَدْخِلْهُ الْجَنَّةَ، وَقِهِ فِتْنَةَ الْقَبْرِ وَعَذَابَ النَّارِ.

{ Ewe Allah msamehe dhambi na umstiri na mrehemu (kwa kumuingiza peponi) na muepushe na yenye kuchukiza (adhabu) na msamehe na mpe sehemu mzuri peponi na panua kaburi lake na muoshe kwa maji na barafu na umande (mtakase na madhambi) na msafishe na makosa kama unavyoisafisha nguo nyeupe kutokana na uchafu na mbadilishie nyumba bora zaidi kuliko nyumba yake, na ndugu bora zaidi ya ndugu zake na mke /mume bora zaidi ya mke wake na muingize peponi na mkinge na mitihani ya kaburini na adhabu ya moto }

رواه مسلم (٩٦٣)

Faida: Kama mke au mume wote wataingia peponi makusudio ya kubadilishwa hapa kama walivyosema baadhi ya wanachuoni ni kubadilishwa sifa zao yaani huyo mkeo atakuwa katika muonekano na sifa nzuri zaidi kuliko alivyo hapa duniani na mume pia .

Tutaendelea na dua namba 02 ya kumuombea maiti in shaa Allah, usikose makala namba 05.

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Imeandaliwa: Tarehe 11 – Rabi’ul – aakhir ≈ 26 – November – 2020M. Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

JIUNGE NASI TELEGRAM UPATE FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⤵️ https://t.me/fawaidussalafiyatz •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *