02- Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya tabia za mtoto wa kiislamu

02- Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya tabia za mtoto wa kiislamu

Makala namba 2:

التَّوَاضُعُ:

Unyenyekevu:

قَالَ رَسُوْلُ اللَّٰهِ صَلَى اللَّٰه عَلَيْهِ وَسَلّمَ مَا نَقصَتْ صَدَقَة مِنْ مَال،وَ مَازَادَ اللَّٰهُ عَبْدًا بِعَفْوٍ إِِلَّا عِزَّا،وَمَا تَوَاضَعَ أَحَدٌ لِلَّهِ إِلَّا رَفَعَهُ اللَّٰهُ

Amesema Mtume was Allah – swala na salamu za Allah ziwe juu yake: Sadaka haipunguzi mali, na Allah hakumzidishia mja kutokana na kusamehe kwake isipokua utukufu, na hakunyenyekea yeyote kwa ajili ya Allah isipokua Allah humnyanyua.

رواه مسلم 2588

[ سلسلة براعم بينونة أخلاق الطفل المسلم – ١ ]

Maelezo:

Mzazi /Mlezi inatakikana umuhimize na umjulishe mwanao ubora wa kutoa sadaka, na sadaka haipunguzi mali bali ni sababu ya kupata baraka katika mali yako, na kumsamehe yule aliyekukosea ni sababu ya kupata utukufu, Allah humpa utukufu yule mwenye tabia ya kusamehe, na kuwa na tabia ya kunyenyekea mafundisho ya Allah – aliyetukuka – na pia kuwanyenyekea watu kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah akifanya hivi basi Allah atamnyanyua. Faida ya unyenyekevu ni kunyanyuliwa duniani na akhera. Sadaka haipunguzi Mali hata ukiona imepungua ni kimuonekano tu ila kimaana imezidi, Sadaka ni sababu ya kuzidishiwa mali na kuteremshiwa baraka, na Allah humpa mtoaji sadaka kheri nyingi, Unyenyekevu kwa ajili ya Allah unamaana mbili (2);

1 – kuzinyenyekea sheria za Allah ukawa hufanyi kibri katika dini wa hufanyi kibri katika kutekeleza hukumu za dini.

2 – kuwanyenyekea waja wa Allah kwa ajili ya Allah si kwa kuwaogopa wala kutaraji kupewa chochote lakini ni kwa ajili ya kutaka radhi za Allah tu. Na kuwa mnyenyekevu na kutokuwa na kiburi ni sababu za kunyanyuliwa duniani na akhera. Na kusamehe unapokosewa kuna kheri nyingi. Usikose makala namba 3, in Shaa Allah..

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Imeandaliwa: Tarehe 06/ Jumaadal-ulaa, 1442H ≈ 21/December, 2020M.

Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

JIUNGE NASI TELEGRAM KUPATA FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⤵️ https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/Darasazandoa •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *