05- Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya tabia za mtoto wa kiislamu
Makala namba 5:
التّعَاوُنُ:
Kusaidiana:
قَالَ رَسُوْلُ اللَّٰهِ صَلَى اللّٰهِ عَلَىيْهِ وسَلّمَ:
Amesema Mtume – swala na salamu za Allah ziwe juu yake:
“الْمُؤمِنُ لِلْمُؤْمِنِ كَالِبُنْيَانِ يَشُدُّ بَعْضهُ بَعْضًا”
رواه البخاري ( ٤٨١)
” Muumini kwa muumini ni kama vile jengo hushikana lenyewe kwa lenyewe ”
Ameipokea Bukhari hadithi namba (481).
[ سلسلة براعم بينونة أخلاق الطفل المسلم – ٤ ]
Maelezo:
Mzazi/mlezi inatakikana umfahamishe mwanao kuwa waislamu wawe ni ndugu wenye kuoneana huruma, wenye kupendana wanatakiwa wawe kama jengo moja kama unavyoona nyumba haitimii ila kwa kutimia vyote vinavyohitajika kama mlango, dirisha, bati n.k, vile vile waislamu ni kitu kimoja katika mambo yao ya kidini na kidunia wasaidiane katika mema na waepuke mipasuko, na ubaguzi yote haya pamoja na kubainisha makosa na kuyaeleza kwa namna ambayo waislamu wote wawe safi kiitikadi, kiibada, kimiamala na washikamane na dini aliyoifundisha Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie.
Usikose makala namba 6, in Shaa Allah..
Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Imeandaliwa: Tarehe 11/ Jumaadal-ulaa, 1442H ≈ 26/December, 2020M. Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
JIUNGE NASI TELEGRAM KUPATA FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⤵️ https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/Darasazandoa •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•