09- Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya tabia za mtoto wa kiislamu

09- Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya tabia za mtoto wa kiislamu

Makala namba 9:

إِكْرَامُ الضَّيْف:

Kumkirimu mgeni:

قال – صلى الله عليه وسلم-:

مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ باللَّٰهِ واليَوْمِ الآخِرِ فَلْيُكْرِمْ ضَيْفَهُ،

Amesema – swala na salamu za Allah ziwe juu yake -: { Yeyote aliyekuwa anamuamini Allah na siku ya mwisho basi amkirimu mgeni wake }

متفق عليه.

[ سلسلة براعم بينونة أخلاق الطفل المسلم – ٩ ]

Maelezo:

Katika uzuri wa dini yetu ya kiislamu na katika tabia nzuri ni kumfanyia wema mgeni, Na wajibu wa kumhudumia mgeni ni siku tatu, siku ya kwanza yaani mchana wake na usiku hii ndiyo siku ya kumkirimu vinono na mwenyeji ajilazimishe kufanya hivyo hata kama anajogoo lake kubwa basi alichinje ama siku zilizobakia atamlisha chakula chake cha kawaida yaani anachokula yeye mwenyewe. Na tabia ya kukirimu wageni ni tabia ambayo Waarabu walikuwa nayo kabla ya uislamu na walikuwa wakishindana na kujifaharisha kwa hilo, Kama anavyosema mshairi akielezea kawaida ya waarabu kipindi hicho:

ضربوا بمدرجة الطريق قبابهم …

يتقارعون على قرى الضيفان

Wameweka mahema yao njiani…

Wakishindana juu ya kuwalisha (kuwakirimu) wageni.

Usikose makala namba 10, in Shaa Allah..

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Imeandaliwa: Tarehe 19/ Jumaadal-ulaa, 1442H ≈ 03/ Jan, 2021M. Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

JIUNGE NASI TELEGRAM KUPATA FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⤵️ https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/Darasazandoa •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *