12- Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya tabia za mtoto wa kiislamu
Makala namba 12:
الصَّدْقُ:
Ukweli:
قَالَ رَسُوْلُ اللَّٰهِ صَلَى اللّٰهِ عَلَىيْهِ وَسَلّمَ:
Amesema Mtume wa Allah – swala na salamu za Allah ziwe juu yake:
دَعْ مَا يَرِيبُكَ إِلَى مَا لَا يَرِيبُكَ فَإِنَّ الصِّدْقَ طُمَأْنِينَةٌ وَإِنَّ الْكَذِبَ رِيبَةٌ.
Acha yale ambayo yanakutia shaka yaelekee (kuyafanya) ambayo hayakutii shaka na bila shaka ukweli ni utulivu (wa moyo) na uwongo ni shaka.
رواه الترمذي ( ٢٥١٨)
[ سلسلة براعم بينونة أخلاق الطفل المسلم – ١٢ ]
Maelezo:
Mzazi /Mlezi inatakikana umuelezee mwanao kuwa siku zote ayafanye yale yasiyokuwa na shaka na ayaache yale yenye mashaka ambayo uhalali wake haupo wazi, na pia muumini wa kweli akitaka kujua kuwa jambo analolifanya ni la kweli au la kheri au ni la haki, basi moyo wake hutulizana na hustarehe na jambo kama si la haki na kweli moyo wa muumini husitasita na hautulizani. Kwa hiyo muumini wa kweli pindi anapopatwa na utata hurejea katika moyo wake kwa sababu moyo wa muislamu wa kweli /muumini humjulisha katika kheri.
Usikose makala namba 13, in Shaa Allah..
Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Imeandaliwa: Tarehe 27/ Jumaadal-ulaa, 1442H ≈ 11/ Jan, 2021M.
Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
JIUNGE NASI TELEGRAM KUPATA FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⤵️ https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/Darasazandoa •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•