16- Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya tabia za mtoto wa kiislamu
Makala namba 16:
الْابْتِسَامَةُ:
Kutabasamu:
قَالَ رَسُوْلُ اللَّٰهِ صَلَّى اللّٰهُ عَلَيْهِ وَسَلّمَ
Amesema Mtume – swala na salamu za Allah ziwe juu yake:
” لَا تَحْقِرَنَّ مِنَ الْمَعْرُوْفِ شَيْىًٔا،وَلَوْ أَنْ تَلْقَى أَخَاكَ بِوَجْهٍ طَلْقٍ ”
” Usidharau katika wema chochote, japo kwa kukutana na ndugu yako kwa uso wenye bashasha (tabasamu)”
رواه مسلم
[ سلسلة براعم بينونة أخلاق الطفل المسلم – ١٦ ]
Maelezo:
Mzazi /Mlezi mfahamishe mwanao kuwa asidharau chochote katika mema japo kwa kukutana na ndugu yako kwa uso wenye bashasha na tabasamu si kwa uso wenye hasira na ghadhabu na huu ndiyo mwenendo wa Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – kuwa na bashasha na tabasamu wakati wa kukutana na hili huleta mapenzi na kuondoa kiburi na majivuno, na katika hili kuna mahimizo ya kufanya mema sawa sawa yawe mema mengi au machache sawa sawa kwa kutoa mali au kwa tabia njema, na huu ndio mwenendo wa Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – kufanya mema hata kwa kitu kidogo.
Usikose makala namba 17, in Shaa Allah..
Mfasiri: fawaidusalafiya.net Imeandaliwa: Tarehe 06/ Jumaadal-aakhir 1442H ≈ 19/ Jan, 2021M.
Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
JIUNGE NASI TELEGRAM KUPATA FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⤵️ https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/Darasazandoa •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•