سلسلة أحكام الصلاة.
MLOLONGO (MFULULIZO) WA HUKUMU ZA SWALA (NO. 68)
SWALA YA ISTIKHARA: SEHEMU YA TATU [3]
Hukumu ya swala ya Istikhara:
أَجْمَعَ الْعُلَمَاءُ عَلَى أَنَّ الاسْتِخَارَةَ سُنَّةٌ، وَدَلِيلُ مَشْرُوعِيَّتِهَا مَا رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ عَنْ جَابِرٍ – رضي الله عنه قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُعَلِّمُنَا الاسْتِخَارَةَ فِي الأُمُورِ كُلِّهَا كَمَا يُعَلِّمُنَا السُّورَةَ مِنْ الْقُرْآنِ. يَقُولُ: إذَا هَمَّ أَحَدُكُمْ بِالأَمْرِ فَلْيَرْكَعْ رَكْعَتَيْنِ مِنْ غَيْرِ الْفَرِيضَةِ ثُمَّ لِيَقُلْ: اللَّهُمَّ إنِّي أَسْتَخِيرُكَ بِعِلْمِكَ وَأَسْتَقْدِرُكَ بِقُدْرَتِكَ وَأَسْأَلُكَ مِنْ فَضْلِكَ الْعَظِيمِ فَإِنَّكَ تَقْدِرُ وَلا أَقْدِرُ وَتَعْلَمُ وَلا أَعْلَمُ وَأَنْتَ عَلامُ الْغُيُوبِ اللَّهُمَّ إنْ كُنْتَ تَعْلَمُ أَنَّ هَذَا الأَمْرَ خَيْرٌ لِي فِي دِينِي وَمَعَاشِي وَعَاقِبَةِ أَمْرِي أَوْ قَالَ: عَاجِلِ أَمْرِي وَآجِلِهِ فَاقْدُرْهُ لِي وَيَسِّرْهُ لِي ثُمَّ بَارِكْ لِي فِيهِ اللَّهُمَّ وَإِنْ كُنْتَ تَعْلَمُ أَنَّ هَذَا الأَمْرَ شَرٌّ لِي فِي دِينِي وَمَعَاشِي وَعَاقِبَةِ أَمْرِي أَوْ قَالَ: عَاجِلِ أَمْرِي وَآجِلِهِ فَاصْرِفْهُ عَنِّي وَاصْرِفْنِي عَنْهُ وَاقْدُرْ لِي الْخَيْرَ حَيْثُ كَانَ ثُمَّ ارْضِنِي بِهِ. وَيُسَمِّي حَاجَتَهُ.
Wamekubaliana wanachuoni kuwa Istikhara ni suna na dalili ya usuna wake ni yale aliyoyapokea Bukhariy kutoka kwa Jabir – Allah amridhie – amesema: Alikuwa Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – akitufundisha Istikhara katika mambo yote kama anavyotufundisha sura katika Qur’ani. (Alikuwa) akisema: Pindi mmoja wenu akiazimia jambo basi aswali rakaa mbili zisizokuwa za faradhi, Kisha (baada ya kumaliza) aseme: Ewe Allah hakika mimi nataka unichagulie la heri kwa elimu yako na nakuomba unipe uwezo (wa kulifanya hili) kwa uwezo wako, na nakuomba kutokana na fadhila zako kubwa na bila shaka wewe unaweza na wala mimi siwezi na (wewe) unajua na wala (mimi) sijui na wewe ni mjuzi wa yaliyojificha, ewe Allah ikiwa unajua kuwa hili jambo (alitaje hilo jambo) ni heri kwangu katika dini yangu na maisha yangu na ukomo wa jambo langu, Au alisema: dunia yangu na akhera, basi nipe uwezo na niwepesishie kisha nibariki ndani yake, ewe Allah na kama unajua kuwa hili jambo (atalitaja) ni shari kwangu katika dini yangu na maisha yangu na ukomo wa jambo langu, Au alisema: Jambo la dunia yangu au akhera basi liondoshe kwangu na niondoshe katika jambo hilo na nikadirie heri popote ilipo kisha niridhie. Na ataitaja haja yake.
رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ فِي مَوَاضِعَ مِنْ صَحِيحِه (١٢٦٦) وَفِي بَعْضِهَا ثُمَّ رَضِّنِي بِهِ.
[ Ameipokea Al-bukhariy katika sehemu (nyingi) kutuko katika sahihi yake (1166) na katika baadhi ya (matamko yake) kisha niridhie kwa jambo hilo ]
Faida zinazotokana na hadithi hii:
1 – Swala ya istikhara ni suna
2 – Istikhara ni suna katika mambo yote makubwa na madogo kwa sababu huwenda jambo dogo likajengeka juu yake jambo kubwa.
3 – Udhahiri wa hadithi unaonesha kuwa unaweza ukaomba dua ya istikhara baada ya rakaa mbili zozote zisizokuwa za faradhi mfano baada ya rakaa mbili za kabla ya dhuhri n.k
4 – Istikhara inakuwa katika hali ya kutaradadi (kusitasita), mfano: unapotaka kufanya biashara kwa kushirikiana na mtu fulani ukawa unajiuliza je, nishirikiane na huyu mtu katika biashara au nisishirikiane naye? muda huu ataswali istikhara.
5 – Hakuwajibiki kusoma sura maalumu katika hizi rakaa mbili.
Itaendelea in shaa Allah, Usikose sehemu ya nne [4].
Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Imeandaliwa: Tarehe 07/ Jumaadal-aakhir 1442H ≈ 20/ Jan, 2021M.
Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
JIUNGE NASI TELEGRAM KUPATA FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⬇️ https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/Darasazandoa •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•