Swala ya Istikhara sehemu ya nne [4]

سلسلة أحكام الصلاة.

MLOLONGO (MFULULIZO) WA HUKUMU ZA SWALA (NO. 69)

SWALA YA ISTIKHARA: SEHEMU YA NNE [4]

مَتَى يَبْدَأُ الاسْتِخَارَةَ؟

Muda gani inaanza istikhara?

Muislamu anatakiwa aswali istikhara pindi pale moyo wake atakapoegemea kulifanya jambo fulani lakini akawa anataradadi /anasitasita yaani bado haja azimia kulifanya asiingie katika istikhara hali ya kuwa moyo wake umeshaazimia kulielekea jambo hilo. kwa kauli yake Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie:

“إذا هم أحدكم ”

“Pindi atakapokusudia mmoja wenu ”

Hii ni dalili kuwa istikhara huswaliwa pindi mtu atakapokusudia tu kulifanya hilo alilokusudia kulifanya kabla ya kumakinika katika moyo yaani pindi yatakapomjia yale mawazo na moyo ukaegemea pamoja na kutaradadi /kusitasita.

Mfano: Mtu anapotaka kuoa baada ya kumuona mchumba kabla ya kukata na kuamua moja kwa moja kuoa basi aswali istikhara, au anataka kufanya aina fulani ya biashara lakini moyo wake unasisita basi muda huo aswali istikhara .n.k Itaendelea in shaa Allah,

Usikose sehemu ya tano [5].

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Imeandaliwa: Tarehe 16/ Jumaadal-aakhir 1442H ≈ 29/ Jan, 2021M.

Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

JIUNGE NASI TELEGRAM KUPATA FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⬇️ https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/Darasazandoa •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *