01 – Mtiririko/ Mfululizo wa kujifundisha adabu za Mtume wa Allah swala na salamu za Allah ziwe juu yake

01 – Mtiririko/ Mfululizo wa kujifundisha adabu za Mtume wa Allah swala na salamu za Allah ziwe juu yake

Makala namba 01:

الأَكْلُ بِالِيَمِيْنِ ( ١)

(1) Kula kwa kutumia mkono wa kulia;

قالَ رَسولُ اللَّهِ – صَلَّى اللهُ عليه وسلَّمَ:

Amesema Mtume – swala na salamu za Allah ziwe juu yake:

يا غُلَامُ، سَمِّ اللَّهَ، وكُلْ بيَمِينِكَ، وكُلْ ممَّا يَلِيكَ

Ewe kijana mtaje Allah (Bismillah) na kula kwa mkono wako wa kulia na kula kinachokuelekea.

رواه البخاري (٥٣٧٦)

Maelezo:

Mzazi /Mlezi mfundishe mtoto wako: Mwanangu katika adabu za kula ambazo ametufundisha Mtume wetu- swala na salamu za Allah zimfikie – ni hizi ambazo Mtume wetu – swala na salamu zimfikie – alimfundisha Umar bin Abii Salamah: Unapoanza kula sema “Bismillah ” na pia kula kwa mkono wako wa kulia na wala usile kwa mkono wa kushoto kama shetani, na unapokula kula chakula kinachokuelekea na wala usimege huku na huku na wala usile katikati ya chakula.

Tanbihi kwa Mzazi /Mlezi:

Katika faida za kumfundisha mtoto adabu hizi za kiislamu ni mtoto kukua nazo na kudumu nazo mfano huyu Umar bin Abii Salamah ambaye alifundishwa mafundisho haya na Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – alisema:

فَما زَالَتْ تِلكَ طِعْمَتي بَعْدُ.

“Basi niliendelea kushikamana na amri ya (Mtume) tokea nilipomsikia”.

Mtiririko huu ni wenye kuendelea Allah akitaka, Usikose namba mbili [2].

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Tembelea website yetu: ☟ https://www.fawaidusalafiya.net

Telegram bonyeza hapa: ☟ https://t.me/fawaidussalafiyatz 🗓️

Imechapishwa: February 16, 2021M, Rajab 4, 1442H.

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

JIUNGE NASI TELEGRAM UPATE FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⬇️ https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/Darasazandoa •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *